Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

16 juni 2021

Karibu usikilize Jarida hii leo ambapo Assumpta Massoi anakufahamisha kuhusu siku ya Umoja wa Mataifa ya Utumaji fedha na hali ilivyo, japo bado dunia inapambana na janga la Corona au COVID-19. Pia leo ni siku ya Mtoto wa Afrika, huko  nchini Niger Benki ya Dunia inasema asilimia 99 ya watoto chini ya miaka 10 hawajui kusoma na kuandika. 

Sauti
12'9"

15 juni 2021

Assumpta Massoi hii leo anaanza jarida kwa kuangazia ripoti ya Shirika la Umoja wa Maraifa la Ajira ambao limetoa ripoti mpya hii leo ikionesha licha ya muongo mmoja wa uwepo wa mkataba wa kimataifa wa haki za wafanyakazi wa ndani,  bado kada hiyo inaendelea kupigania usawa na mazingira bora ya kazi huku janga la ugonjwa wa Corona au COVID19 likionesha dhahiri udhaifu uliopo katika kada hiyo.

Sauti
13'4"

11 Juni 2021

Na sasa ni mada kwa kina, kama nilivyokudokeza hapo awali, kuelekea siku ya kimataifa ya kuelimisha jamii kuhusu watu wenye ualbino tarehe 13 mwezi huu wa Juni, Umoja wa Mataifa unaelezea mshikamano wake na watu wenye ualbino. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antoni Guterres anasema kauli mbiu ya mwaka huu, uthabiti licha ya mazingira magumu,  ‘ni kielelezo cha uthubutu, ustahimilivu na hatua za watu wenye ualibino katika mazingia ya habari  potofu, unyanyapaa na ukatili. 

Sauti
14'7"

10 Juni 2021

Hii leo katika jarida Leah Mushi anaanza na ripoti ya ajira za watoto duniani ikielezwa kuwa ajira za utotoni zimefikia milioni 160, zaidi ya nusu ni watoto wa wenye umri wa miaka 5 hadi 11. Kisha anamulika suala la ukeketaji ambapo mwanaharakati dhidi ya ukeketaji, Ifrah anasema katu hatopumzika hadi maghariba waweke chini visu na nyembe zao. Huko Ethiopia nako anabisha hodi kwa kuwa UNICEF na serikali wanasaidia kaya maskini za mijini kwa kupatia fedha za kujikimu.

Sauti
13'9"

09 Juni 2021

Hii leo Leah Mushi anaanza na mashindano ya michezo Olimpiki yanayoanza mwezi ujao huko Tokyo Japan ambako wakimbizi watashikiri. Kisha anabisha hodi DRC jimboni Katanga Juu kukutana na watoto walionusuriwa kutoka uchimbaji madini. Safari yake itaendelea hadi Ethiopia kwa vijana wanaotekeleza  mradi kwa ufadhili wa IFAD. Mashinani ni nchini Iraq kauli ya mkimbizi aliyerejea nyumbani na kukuta hali si hali. Makala tunamulika ujauzito katika umri mdogo kutoka kwa John Kabambala. Karibu!

Sauti
13'8"

08 JUNI 2021 B

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Leah Mushi anakuletea 

-Leo ni siku ya ya Bahari duniani, katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake wa maadhimisho ya siku hii, ametoa wito wa kuacha kuchafua bahari kwani inaathiri zaidi wanufaika wake ambao wengi ni wafanyabiashara wadogo kutoka nchi zinazo endelea.

-Tanzania imechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA utakaoanza tarehe mosi mwezi Septemba mwaka huu na pia mjumbe wa ECOSOC kuanzia mapema mwaka 2022

Sauti
12'18"

07 Juni 2021

Leo Jumatatu ni Mada kwa Kina na kwa kuwa ni siku ya Umoja wa Mataifa ya usalama wa chakula duniani, tunamulika usalama wa chakula unachokula.  Shirika la Umoja wa Mataifa la Kilimo na Chakula -FAO limesema iwapo chakula anachokula mlaji wa mwisho kimepitia kwenye namna yoyote inayoweza kuhatarisha usalama wake ikiwemo kupata magonjwa basi hicho hakistahili kuitwa chakula. 

Sauti
13'35"

04 JUNI 2021

Katika jarida la mada kwa kina kutoka Umoja wa Mataifa hii leo Leah Mushi anakuletea:

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema mashambulizi makali yanayotekelezwa na wapiganaji wa kundi la Allied Democratic Forces ADF, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC yamewalazimisha takriban watu 5,800 kukimbia mara kadhaa katika makazi ya watu waliotawanywa katika jimbo la Ituri Mashariki mwa nchi hiyo

Sauti
12'19"

03 JUNI 2021

Hii leo jaridani tunaanza na mfumo mpya wa malipo kwa wakulima nchini Uganda kupitia MobiPay ambako sasa wakulima hawakopwi tena. Kisha suala la hedhi na changamoto zake kwa wakimbizi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Na siku ya baiskeli duniani leo tumekwenda Mwanza nchini Tanzania kuzungumza na waendesha baiskeli. Makala tunakwenda tena Uganda ambako wananchi wanataka wabunge wapya wasaidie kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Mashinani tunaelekea Sudan Kusini kwake Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Karibu!

Sauti
14'40"

02 JUNI 2021

Hii leo jaridani Leah Mushi anaanzia huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako waasi wa ADF wameshambulia kambi za wakimbizi wa ndani na kuua raia 55, UN umetoa taarifa ya kulaani. Atasalia huko huko Maziwa Makuu akimulika wakimbizi waliongia nchini Rwanda wakikimbia volkano ya Nyiragongo huko DRC na kisha atamulika pia suala la ndoa za utotoni. Makala tunamkaribisha John Kibego kutoka Uganda na mashinani ni ujumbe kutoka UNAIDS, karibu!