Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

04 JUNI 2021

04 JUNI 2021

Pakua

Katika jarida la mada kwa kina kutoka Umoja wa Mataifa hii leo Leah Mushi anakuletea:

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema mashambulizi makali yanayotekelezwa na wapiganaji wa kundi la Allied Democratic Forces ADF, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC yamewalazimisha takriban watu 5,800 kukimbia mara kadhaa katika makazi ya watu waliotawanywa katika jimbo la Ituri Mashariki mwa nchi hiyo

-Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA leo imezindua mpango wa kukabiliana na  mahitaji ya kibinadamu kwa ajili ya Chad ambako watu milioni 5.5 wanahitaji msaada wa kibinadamu.  

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo limesema linaendelea kutiwa hofu na taarifa za kulazimishwa kurejea nyumbani kwa familia kutoka Msumbiji zilizokimbilia Tanzania. 

-Mada yetu kwa kina leo inamulika uzinduzi wa muongo wa kurejesha ikolojia ikiwa ni katika kuelekea siku ya mazingira duniani inayoadhimishwa kila mwaka Juni 5.

-Na katika kujifunza Kiswahili leo tuko Uganda kwa  mwenyekiti wa idara za Kiswahili katika vyuo vikuu Afrika Mashariki Aida Mutenyo anatufafanulia maana ya msemo "MSIBA HUAMBATANA NA MSIBA MWENZIE"

Audio Credit
UN News/Leah Mushi
Audio Duration
12'19"