Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

10 Juni 2021

10 Juni 2021

Pakua

Hii leo katika jarida Leah Mushi anaanza na ripoti ya ajira za watoto duniani ikielezwa kuwa ajira za utotoni zimefikia milioni 160, zaidi ya nusu ni watoto wa wenye umri wa miaka 5 hadi 11. Kisha anamulika suala la ukeketaji ambapo mwanaharakati dhidi ya ukeketaji, Ifrah anasema katu hatopumzika hadi maghariba waweke chini visu na nyembe zao. Huko Ethiopia nako anabisha hodi kwa kuwa UNICEF na serikali wanasaidia kaya maskini za mijini kwa kupatia fedha za kujikimu. Makala ni kuhusu apu ya simu iliyobuniwa nchini Kenya na Peninah Wanja ikipatiwa jina DigiCow kwa lengo la kusaidia wafugaji ng’ombe kupata huduma muhimu kwa njia rahisi. Na kutoka mashinani tunakwenda kwa mwandishi wa vitabu vya watoto Stacey Fru, karibu!

Audio Duration
13'9"