Assumpta Massoi hii leo anaanza jarida kwa kuangazia ripoti ya Shirika la Umoja wa Maraifa la Ajira ambao limetoa ripoti mpya hii leo ikionesha licha ya muongo mmoja wa uwepo wa mkataba wa kimataifa wa haki za wafanyakazi wa ndani, bado kada hiyo inaendelea kupigania usawa na mazingira bora ya kazi huku janga la ugonjwa wa Corona au COVID19 likionesha dhahiri udhaifu uliopo katika kada hiyo.