Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

08 JUNI 2021 B

08 JUNI 2021 B

Pakua

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Leah Mushi anakuletea 

-Leo ni siku ya ya Bahari duniani, katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake wa maadhimisho ya siku hii, ametoa wito wa kuacha kuchafua bahari kwani inaathiri zaidi wanufaika wake ambao wengi ni wafanyabiashara wadogo kutoka nchi zinazo endelea.

-Tanzania imechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA utakaoanza tarehe mosi mwezi Septemba mwaka huu na pia mjumbe wa ECOSOC kuanzia mapema mwaka 2022

-Nchini Bangladesh taka ngumu ikiwemo plastiki ni mtihani mkubwa ambao shirika la Umoja wa Mataifa IOM umeuvalia njia kwa suluhu mbadala

-Makala yetu leo inatupeleka Uganda ambako shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women inawasaidia wanawake kujikwamua na kukabiliana na changamoto zinazowakabili

-Na mashinani tutakuwa Burkina Faso kumsikia muhudumu wa masuala ya kibinadamu wa shirika la Umoja wa Mataifa OCHA akizungumzia wanachofanya kusaidia jamii zilizoathirika na vita

Audio Credit
UN News/Leah Mushi
Audio Duration
12'18"