Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

11 Juni 2021

11 Juni 2021

Pakua

Na sasa ni mada kwa kina, kama nilivyokudokeza hapo awali, kuelekea siku ya kimataifa ya kuelimisha jamii kuhusu watu wenye ualbino tarehe 13 mwezi huu wa Juni, Umoja wa Mataifa unaelezea mshikamano wake na watu wenye ualbino. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antoni Guterres anasema kauli mbiu ya mwaka huu, uthabiti licha ya mazingira magumu,  ‘ni kielelezo cha uthubutu, ustahimilivu na hatua za watu wenye ualibino katika mazingia ya habari  potofu, unyanyapaa na ukatili. 
Guterres anapigia chepuo uongozi wa mashirika ya kutetea watu wenye ualbino na hata wao wenyewe kuwa mstari wa mbele ingawa kuna wakati wanakuwa hatarini.
Mgeni wetu kwenye mada kwa kina hii leo ni dhihirisho la ushindi licha ya changamoto kama alivyosema Guterres. Na mgeni wetu kutoka Kenya amezungumza na Grace Kaneiya akiwa Nairobi Kenya. Kwako Grace  ukumbi ni wako.
 

Audio Credit
Leah Mushi/Grace Kaneiya
Audio Duration
14'7"