Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

07 Juni 2021

07 Juni 2021

Pakua

Leo Jumatatu ni Mada kwa Kina na kwa kuwa ni siku ya Umoja wa Mataifa ya usalama wa chakula duniani, tunamulika usalama wa chakula unachokula.  Shirika la Umoja wa Mataifa la Kilimo na Chakula -FAO limesema iwapo chakula anachokula mlaji wa mwisho kimepitia kwenye namna yoyote inayoweza kuhatarisha usalama wake ikiwemo kupata magonjwa basi hicho hakistahili kuitwa chakula. 

Nchini Tanzania, Ahimidiwe Olutu kutoka kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa UNIC jijini Dar es salaam amezungumza na wafanyabiashara na wananchi wa kawaida kufahamu Je, wanafanya nini kujihakikishia usalama wa chakula chao kila siku? Na katika mashinani tunasalia huko huko Tanzania. Karibu na mwenyeji wako jaridani leo ni Leah Mushi.

Audio Duration
13'35"