Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

16 Aprili 2021

16 Aprili 2021

Pakua

Umoja wa mataifa unaamini kuwa michezo licha ya kuwa chanzo cha kipato na afya, ina mchango mkubwa katika kuleta maendeleo na amani kwani kupitia michezo watu walio na tofauti mbalimbali za kijamii, wanaweza kukutana, kuondoa tofauti zao na hatimaye kushiriki katika ujenzi wa maendeleo bila kukwamishwa na tofauti zao. Ndio maana watu duniani kote wanahamasishwa kuutokomeza ugonjwa wa Civid-19, ili viwanja vya michezo vifufuke tena. Kutoka Bujumbura Burundi, washirika wetu Mashariki TV wametuandalia makala hii inayoeleza namna ambavyo michezo imefanikisha hilo nchini Burundi. Makala inasimuliwa na Harumukiza Edmond. 

Audio Duration
11'59"