Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

26 Aprili 2021

26 Aprili 2021

Pakua

Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP mwaka 2017 lilizindua kampeni ya bahari safi au CleanSeas kwa lengo la kushirikisha serikali, umma, mashirika ya kiraia na sekta binafsi katika kutokomeza utupaji taka kwenye maeneo ya bahari na maziwa. Tangu wakati huo kampeni hiyo imekuwa moja ya kampeni kubwa duniani ya kuondokana na taka za plastiki baharini ambapo hata watu binafsi wametumia ubunifu wao kuibuka na mbinu za kuondokana na taka hizo baharini. Miongoni mwao ni watengenezaji wa ngalawa iliyotumia taka za plastiki na kandambili na kisha kusafiri kutoka Kisumu upande wa Kenya hadi Mwanza Tanzania na kisha kusafirishwa hadi dar es salaam ili kusambaza ujumbe wa kusafisha fukwe na kutotumia plastiki. Ni kwa vipi basi, Lucy Igogo wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC Dar es salaam nchini Tanzani ameandaa mada hii kwa kina.

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
11'52"