Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

30 APRILI 2021

30 APRILI 2021

Pakua

Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo ikiwa ni mada kwa kina Grace Kaneiya anakuletea 

-Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuhusu ukimwi imependekeza masuala 10 ya kuzingatia kutokomeza janga hilo ifikapo 2030 na kutimiza ajenda ya SDGs.

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA limeelezea kusikitishwa kwake na athari za ongezeko la mashambulizi dhidi ya wahudumu wa misaada ya kibinadamu nchini Sudan Kusini

-Mashirika ya Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na lile la kimataifa la uhamiaji IOM wamesema machafuko huko Cabo del Gado Msumbiji yanaendelea kuwalazimisha raia kufungasha virago na kukimbia makwao wengi wakiwa wanawake na watoto

-Mada kwa kina leo inatupeleka Burundi kuangazia juhudi zinazofanyika kwa watu wenye ulemavu kusaidiana na kusongesha ajenda ya Umoja wa Mataifa ya ujumuishwaji wa watu wenye ulemavu katika nyanja mbalimbali kwenye jamii

-Na katika kujifunza Kiswahili leo tutakuwa Uganda kwa kwenyekiti wa idara za Kiswahili za vyio vikuu wa Afrika Mashariki Ida Mutenyo akifafanua maana za neno barabara

 

Audio Credit
UN News/Grace Kaneiya
Audio Duration
12'20"