Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

08 DESEMBA 2023

Hii leo kwenye jarida Assumpta Massoi anamulika mzozo Mashariki ya Kati hususan huko Gaza,  nyaya za simu zageuzwa kuni, kisha anakwenda Mashariki mwa Afrika huko baada ya ukame wa muda mrefu sasa ni mvua za kupindukia zinazosababisha maafa makubwa,; makala anakupeleka Tanzania kusikia uchambuzi wa Ibara ya 15 ya Tamko la Haki za Binadamu la UN, na mashinani utamsikia binti shujaa wa mazingira kutoka visiwani Zanzibar nchini Tanzania.

Sauti
9'45"

07 DESEMBA 2023

Hii leo kwenye jarida Leah Mushi anakuletea Habari kwa Ufupi ikiangazia Tanzania, janga la chakula Afrika na Mkutano wa UN na wanazuoni. Katika Mada kwa Kina tunamulika mshindi wa Tuzo ya UN ya Haki za Binadamu Julienne Lusenge kutoka DRC na Jifunze Kiswahili maana ya neno, Kifandugu.

Sauti
11'41"
COP28

Solar Sister watekeleza kwa vitendo nishati safi kwa jamii za pembezoni

Kila uchao, sauti zinapazwa kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, tena hasa wakati huu ambapo wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mabadiliko ya Tabianchi, UNFCCC wakikutana Dubai, huko Falme za Kiarabu kwenye mkutano wao wa 28 au COP28. Tayari  hatua zimechukuliwa na shirika la kimataifa la Solar Sister kusaka nishati salama hasa kwa wanawake wa vijijini kama anavyoshuhudia mwanachama na mnufaika wake, Loveness Sabaya wa jamii ya kimasai kutoka Arusha nchini Tanzania kupitia video iliyochapishwa kwenye ukurasa wa X wa mkutano wa COP28. 

Sauti
1'39"
©UNICEF/UNI472270/Zaqout

Uchunguzi ufanywe Gaza kuhusu madai ya ukatili wa kingono wakati wa shambulio la Hamas - OHCHR

Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk leo amelaani vikali ukiukaji mkubwa wa haki wa kingono dhidi ya Waisraeli unaodaiwa kutekelezwa na wanamgambo wa Hamas wakati wa mashambulizi yao ya kigaidi kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba, huku wahudumu wa kibinadamu huko Gaza wakionya kuhusu hali mbaya ya raia. 

Kamishina mkuu Türk akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis amesisitiza kuhusu hofu yake kwa hatma ya raia akirejea wito wa kukomesha uhasama mara moja kunusuru Maisha ya raia na miundombinu yao. 

Sauti
1'53"
UN News/Dominika Tomaszewska-Mortimer

Walio hatarini zaidi waletwe ‘mbele ya mstari’ wa ufadhili wa tabianchi - COP28

Leo huko Dubai, UAE kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mazingira, COP28, Akaunti ya Hatua Dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi imezinduliwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu na Masuala ya Dharura (OCHA) ili kutoa njia ya ziada ya kufadhili hatua za kibinadamu kwenye majanga yanayohusiana na tabianchi kama vile mafuriko, ukame, dhoruba na joto kali, na kujenga uwezo wa kustahimili tabianchi. 

Sauti
2'6"
Public Health Alliance/Ukraine

Katika kutokomeza VVU mchango wa jamii hasa vijana unahitajika sana - Jane

Leo ni siku ya ukimwi duniani ambapo mwaka huu shirika la Umoja wa Mataifa la kukabili ukimwi UNAIDS limetenga maudhui kuwa “Achia Jamii Ziongoze” kwa lengo la kuzisihi serikali kote duniani kutumia ipasavyo nguvu ya jamii mashinani ili hatimaye kutokomeza ugonjwa wa Ukimwi ifikapo mwaka 2030  huku Afrika Kusini mwa Janga la Sahara ikitajwa kuwa muathirika mkumbwa wa maambukizi mapya ya VVU. 

Sauti
3'17"
© UNICEF

Mafuriko makubwa yaathiri wenyeji Somalia baada ya ukame wa miaka minne mfululizo

Mkutano wa COP28 ukiendelea Dubai, Falme za kiarabu kusaka suluhu dhidi ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi, huko Somalia mafurikio makubwa yameendelea kusababisha zahma kwa wananchi ambapo Umoja wa Mataifa kupitia ofisi yake ya uratibu wa misaada ya dharura, OCHA umezungumzia hali halisi na nini kinafanyika. 

Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwa njia ya mtandao  kutokea Mogadishu,Somalia, OCHA imebainisha kuwa  Somalia inakabiliana na mafuriko yaliyoyaathiri maeneo mengi. 

Sauti
2'3"
WHO / Christopher Black

COP28 ihakikishe inamulika jinsi ya kupunguza vifo vitokanavyo na janga la tabianchi- WHO

Kuelekea mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP28 huko Dubai, Falme za kiarabu tarehe 30 mwezi huu wa Novemba, shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO, limesema washiriki wanapaswa waelewe kuwa suala la afya ndilo linapaswa kuchochea majadiliano wakati huu ambapo janga la tabianchi linazidi kushamiri duniani kote. 

Sauti
2'23"