Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katika kutokomeza VVU mchango wa jamii hasa vijana unahitajika sana - Jane

Katika kutokomeza VVU mchango wa jamii hasa vijana unahitajika sana - Jane

Pakua

Leo ni siku ya ukimwi duniani ambapo mwaka huu shirika la Umoja wa Mataifa la kukabili ukimwi UNAIDS limetenga maudhui kuwa “Achia Jamii Ziongoze” kwa lengo la kuzisihi serikali kote duniani kutumia ipasavyo nguvu ya jamii mashinani ili hatimaye kutokomeza ugonjwa wa Ukimwi ifikapo mwaka 2030  huku Afrika Kusini mwa Janga la Sahara ikitajwa kuwa muathirika mkumbwa wa maambukizi mapya ya VVU. 

Kwa mujibu wa takwimu za UNAIDS za mwaka huu 2023 wasichana vigori na vijana walichangia zaidi ya asilimia 77 ya maambukizi mapya ya VVU Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara mwaka jana 2022 miongoni mwa vijana wenye umri wa miaka 15-24.

Na wasichana wana uwezekano mara tatu zaidi ya kupata VVU kuliko wenzao wa kiume. 

Kenya ikiwa ndani ya nchi 15 zenye maambukizi makubwa ya VVU Afrika juhudi kubwa zinafanywa kupitia serikali, asasi za kiraia na hata watu binafsi kusongesha mbele vita dhidi ya VVU kwa msaada wa wadau mbalimbali wa kitaifa na kimataifa ukiwemo Umoja wa Mataifa ambao leo katia kuadhimisha siku hii jijini Nairobi umeandaa mashindano ya riadha ya kilometa 5 na kuchangisha fedha zitakazowasaidia yatima wa ugonjwa huo kama anavyofafanua Jane Sinyei Afisa Uratibu Msaidisi wa ofisi ya Umoja wa Mataifa Nairobi UNON.

“Zile fedha ambayo tutapata itaenda kusaidia watoto wale wasio na wazazi, wasio na kitu chochote hivyo tutakuwa tunafanya kazi ya kusaidia wasiojiweza. Pia tutafanya vipimo vya VVUnkwa wale ambao watakuwa na virudsi hivyo wataelimishwa jinsi ya kufika kwa madaktari, kupata dawa na kwa wale ambao hawatakuwa na virusi vya ukimwi wataelimishwa jinsi ya kuendelea kujikinga na VVU ili wazuie kupata ukimwi na kusambazia wengine ukimwi.” 

Jane ana ujumbe kwa vijana ambao ndio kundi kubwa la waathirika wa VVU

“Vijana tunawasihi mje msitari wa mbele , nyinyini viongozi wa leo na kesho na hapa Kenya mko wengi sana kuliko sisi. Mje mjifunze jinsi mtakavyojikinga na ukimwi, Homa ya ini aina B na magonjwa ya zinaa, na kuelimisha arafiki zenu ili wajikinge na haya magonjwa, muwe na afya bora ili muongize watu wote katika hii nchi yetu.”

Nchi za Afrika zinazoongoza kwa VVU kwamujibu wa UNAUDS ni Eswatini inayoshika namba moja ikifuatiwa na Lesotho, Botswana na Zimbabwe. Tanzania inashika namba 11, Kenya 12 na Uganda ya 13.

Audio Credit
Leah Mushi
Sauti
3'17"
Photo Credit
Public Health Alliance/Ukraine