Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

08 DESEMBA 2023

08 DESEMBA 2023

Pakua

Hii leo kwenye jarida Assumpta Massoi anamulika mzozo Mashariki ya Kati hususan huko Gaza,  nyaya za simu zageuzwa kuni, kisha anakwenda Mashariki mwa Afrika huko baada ya ukame wa muda mrefu sasa ni mvua za kupindukia zinazosababisha maafa makubwa,; makala anakupeleka Tanzania kusikia uchambuzi wa Ibara ya 15 ya Tamko la Haki za Binadamu la UN, na mashinani utamsikia binti shujaa wa mazingira kutoka visiwani Zanzibar nchini Tanzania.

  1. Wakati mashambulizi ya Israel yakiendelea kushika kasi huko Ukanda wa Gaza na mapigano na makundi yaliyojihami ya kipalestina yakiwa kikwazo kikubwa cha kusambaza misaada ya kibinadamu, Umoja wa Mataifa leo umeonya kwamba jamii inakaribia kusambaratika kabisa watu wakifikia hatua ya kukata nyaya za simu za kuzitumia kama kuni. Taarifa ni ya Flora Nducha.
  2. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) linaonya kuwa mafuriko makubwa yanatishia kuongeza zaidi tatizo la kukosekana kwa uhakika wa kupatikana kwa chakula katika eneo la Mashariki mwa Afrika licha ya kwamba shirika hilo linajitahidi kusambaza misaada. Anold Kayanda ndiye ameandaa ripoti hii.
  3. Makala inamulika ibara ya 15 ya Tamko la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu ambalo mwaka huu linatimiza miaka 75. Mchambuzi wetu ni Mhadhiri na mwanasheria wa Haki za Binadamu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino SAUT mkoani Mwanza, Kaskazini-Magharibi mwa Tanzania Shukuru Paul, akihojiwa na Evarist Mapesa wa Idhaa hii.
  4. Na mashinani fursa ni yake Nasra, binti huyu shujaa wa mazingira kutoka Zanzibar nchini Tanzania, ambaye ni kiongozi mwenye shauku wa klabu yake ya shule ya upandaji miti na anatumia sauti yake kuhamasisha watu kutunza mazingira na kuhakikisha ulimwengu ulio endelevu zaidi siku za usoni.  Karibu!
Audio Credit
ASSUMPTA MASSOI
Audio Duration
9'45"