Nchini Colombia, mashambulio ya bomu yameripotiwa hii leo kwenye bomba la kusafirisha mafuta la Cano Limon katika majimbo ya Arauca na Boyaca, ikiwa ni siku moja tu baada ya kumalizika kwa muda wa makubaliano ya muda ya kusitisha mapigano kati ya serikali na kikundi cha National Liberation Army, ELN.

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Colombia, Jean Arnault ametoa taarifa hizo mbele ya wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo jijini New York, Marekani wakati akiwasilisha ripoti kuhusu harakati za Umoja wa Mataifa za kusimamia amani Colombia.
Amesema mashambulio hayo yametokea wakati huu ambapo mazungumzo yanafanyika huko Quito kati ya serikali na ELN.
(Sauti ya Jean Arnault)
“Twatumai kuwa mazungumzo huko Quito yataibuka na matokeo mazuri kukidhi matarajio na tunapendekeza muda zaidi, siyo muda mrefu sana bila shaka, kwa Katibu Mkuu awasilishe mapendekezo yake kwa Baraza kwa kuzingatia mjadala huu.”

Bwana Arnault amesema sitisho hilo la mapigano ni jambo linalopigiwa chepuo na pande zote nchini Colombia akisema..(Sauti ya Jean Arnault)
“Nchini Colombia ari ya kuona sitisho la muda la mapigano linaendelea limekubaliwa kwa kauli moja bila kujali changamoto ambazo zimekuwepo.”
Mwakilishi huyo maalum katika ripoti ya Katibu Mkuu akazungumzia pia harakati za kujumuisha tena kwenye jamii wapiganaji wa kikundi cha FARC-EP baada ya kumalizika kwa uhasama kati yao na serikali uliodumu kwa zaidi ya miongo mitano.
Amesema ujumuishaji wa kisiasa unaenda vyema ambapo tayari wapiganaji hao wa FARC-EP wameunda chama kipya na watashiriki uchaguzi wa Bunge na mitaa lakini changamoto ni ujumuishaji wa kiuchumi akisema..
(Sauti ya Jean Arnault)