Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wadau lazima watimize wajibu wao kurejesha amani DRC: Lacroix

MONUSCO yasaidia usafirishaji wa vifaa vya kuandikisha wapiga kura DRC. Picha: MONUSCO (maktaba)

Wadau lazima watimize wajibu wao kurejesha amani DRC: Lacroix

Amani na Usalama

Ili amani ya kweli na ya kudumu iweze kurejea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ni lazima wadau wote wa kisiasa ikiwemo serikali, chama tawala, wapinzani, asasi za kiraia na tume ya uchaguzi watimize wajibu wao katika kuhakikisha maandalizi ya uchaguzi mkuu yanaendelea kwa wakati kama ilivyopangwa.

Wito huo umetolewa na mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix alipotoa taarifa hii leo kwenye baraza la usalama  kuhusu hali nchini DRC na kusisitiza kuwa

(JEAN-PIERRE LACROIX-CUT 1)

“Ni muhimu kwa viongozi wa kisiasa wa DRC kuzingatia Katiba, mkataba wa kisiasa wa 31 Disemba 2016 na kalenda ya uchaguzi, ambayo pamoja, inatoa mfumo wa kisiasa na kisheria kwa ajili ya kuendesha uchaguzi huru , wa haki na wa kuaminika, utakaohamisha madaraka kwa njia ya amani na kuimarisha taasisi za kidemokrasia za nchi hiyo.”

Amesema kucheleweshwa kwa aina yoyote ile kwa uchaguzi uajao kutochochea hali ambayo tayari ni mbaya kuwa zahma kubwa na hasa kwa raia ambao amesema mamilioni wanabeba gharama za maisha yao na kulazimika kufungasha virago kuwa wakimbizi wa ndani na nje.

Ameseisitiza kuwa hali ya usalama bado ni tete katika katika maeneo mbalimbali kutokana na machafuko ya wenyewe kwa wenyewe lakini pia kutokana na tishio la waasi kama Mayi-Mayi na pia ADF ambao wanakatili maisha ya raia na walinda amani wakiwemo walinda amani 15 wa Tanzania waliouawa mwezi Disemba huko Semuliki Kivu Kaskazini. Na hivyo

( LACROIS CUT 2)

“Kudhibiti ADF itahitaji ushirikiano wa kikanda, kukusanya taarifa za uchambuzi, kuvuruga mitandao ya misaada ya kisiasa na kiuchumi ya Kundi hilo, na kuimarisha ushirikiano kati ya MONUSCO na vikosi vya kitaifa vya usalama, na shughuli za kijeshi zinazowalenga.”

Ameongoza kuwa uchunguzi ulioanza ambao unaongozwa na msaidizi wa Katibu Mkuu Dimitry Titov utatoa muongozo na mwelekeo wa hatua za kuchukuliwa.

Hata hivyo amesema licha ya changamoto zote hizo hatua zimeanza hususani katika uandikishaji wa wapiga kura na zoezi hilo linatarajiwa kukamilika mwezi Februari.