Guterres kuzungumza na Rais Magufuli wa Tanzania
Kufuatia mauaji ya walinda amani 14 wa Tanzania huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC siku ya Alhamisi na wengine zaidi ya 44 kujeruhiwa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres muda wowote sasa atazungumza kwa njia ya simu na Rais John Magufuli wa Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki nchini Tanzania, Balozi Augustine Mahiga amesema hayo akihojiwa na Idhaa hii kwa njia ya simu kutoka Dar es salaam.
(Sauti ya Balozi Augustine Mahiga)
Balozi Mahiga akazungumzia pia kuhusu hatma ya walinda amani ambao walikuwa hawajulikani waliko.
(Sauti ya Balozi Augustine Mahiga)
Halikadhalika amesema Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix pamoja na msaidizi wake Atul Khare wanatarajiwa kuwasili nchini Tanzania muda wowote.
