Wanahabari watoto wapasha umma kuhusu changamoto za maji DRC kwa kuwezeshwa na UNICEF
Hii leo ni siku ya maji duniani na ninakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako huko mtoto Liesse mwenye umri wa miaka 17 amefuatilia upatikanaji wa maji safi ya kunywa kwenye eneo la Goma jimboni Kivu Kaskaizini baada ya kupatiwa mafunzo ya uandishi wa habari na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF na hatimaye taarifa yake kutangazwa na Radio Okapi ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo.