Huko Goma hii leo kwenye jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO kunafanyika tukio maalum la kuenzi walinda amani 14 wa Tanzania waliouawa katika shambulio wiki iliyopita huku familia za walinda amani hao zikizungumzia mustakhbali wao.
Shughuli hiyo inaongozwa na mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix pamoja na Balozi wa Tanzania nchini DRC Ignace Meela.
Kabla ya kushiriki tukio hilo, Bwana Lacroix aliwajulia hali walinda amani wengine ambao bado wamelazwa kwenye hospitali mjini Goma na kusema...
(Sauti ya Jean-Pierre Lacroix)
“Nimeshiriki katika tukio la kutoa shukrani huko Dar es salaam na leo niko hapa. Nimetoka pia katika tukio lililoandalwa hapa Goma na pia Kampala. Hapa Goma nimetembelea askari wa Tanzania ambaao walijeruhiwa. Nimetakia ahueni ya haraka. Na nimeridhika kuwa wanahudumiwa vizuri na inatia faraja.”

Nako nchini Tanzania wakati maziko ya walinda amani yakifanyika, baadhi ya wanafamilia wamezungumzia mustakhbali wa familia akiwemo Mohammed Khatib ambaye ni mjomba wa mlinda amani Shazil Nandonde.(Sauti ya Mohammed Khatib)

Kwa upande wake Mathilda Wakusola ambaye ni dada wa marehemu Samuel Chenga amesema.(Sauti ya Mathilda Wakusola)
Haji Hassan Hamis kutoka Zanzibar akamzungumzia marehemu Hassan Abdallah Makame ambaye ni mtoto wa dada yake na aliwahi kuhudumu Darfur nchini Sudan na baadaye DRC ambako mauti yalimkuta.
(Sauti ya Haji Hassan Hamis)