Kivu Kaskazini

UNHCR yawajengea nyumba wakimbizi wa ndani DRC

Machafuko yanaendelea Jimbo la Kivu kaskazini nchini Jamhuri ya kidemokrasia Kongo, DRC yanasababisha kila uchwao wananchi wa eneo hilo kuyakimbia makazi yao kwenda kuishi mikoa ya jirani.

Mashambulizi mashariki mwa DRC yafurusha watu 20,000 

Mashambulizi dhidi ya raia huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC yamesababisha watu 20,000 kukimbia makazi yao licha ya hatua ya Rais Felix Tshisekedi ya kutangaza hali ya hatari katika majimbo ya Ituri na Kivu Kaskazini tarehe 6 mwezi Mei mwaka huu. 

UNICEF yawezesha wakazi wa Goma nchini DRC kunywa maji masafi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linahaha kurejesha huduma ya maji safi na salama kwa wakazi 200,000 wa mjji wa Goma jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC baada ya huduma hiyo kuharibiwa na mlipuko wa volkano kwenye mlima Nyiragongo tarehe 22 mwezi uliopita wa Mei.
 

Waasi DRC wavamia kambi za wakimbizi wa ndani na kuua raia 55, UN yapaza sauti

Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali mashambulio ya siku ya Jumatatu yaliyofanywa na waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) dhidi ya wakimbizi wa ndani hu

Sauti -
1'17"

Volkano ya Nyiragongo imesambaratisha maisha yetu- Mkimbizi kutoka DRC 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na wadau wengine wanawasaidia watu waliolazimika kuyakimibia makazi yao baada ya mlipuko wa volkano katika Mlima Nyiragongo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC. Wengi walivuka mpaka kwenda nchi jirani ya Rwanda ambako sasa wanapata usaidizi.

UN yalaani mauaji ya raia 55 yaliyofanywa na ADF mashariki mwa DRC 

Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali mashambulio ya siku ya Jumatatu yaliyofanywa na waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) dhidi ya wakimbizi wa ndani huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na kusababisha vifo vya raia 55 na wengine wengi wamejeruhiwa.

Poleni DRC kwa janga la mlipuko wa volkano Mlima Nyiragongo- Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameeleza masikitiko yake kufuatia vifo, majeruhi na uharibifu wa mali uliosababishwa na mlipuko wa volkano katika mlima Nyiragongo, huko Goma jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Tunalaani vikali shambulio dhidi ya MONUSCO Kivu Kaskazini:UN 

Umoja wa Mataifa umelaani vikali shambulio lililofanyika jana Jumatatu dhidi ya eneo la muda la mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC katika mji wa Beni jimboni Kivu Kaskazini. 

Wananchi wapongeza juhudi za UN kurejesha amani zapongezwa DRC

Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi hao Sheikh Abdul Kambale Bageni wa msikiti wa Mutwanga na Padri Ghislain Katsere wa Parokia ya Mutwanga  wanasema wanasema ulinzi wa amani kutoka Umoja wa Mataifa umesaidia sana kurejesha maisha katika hali yake ya kawaida na sasa watu wameanza kuishi bil

Sauti -
2'35"

Juhudi za UN kurejesha amani zapongezwa DRC

Shughuli za ulinzi wa amani zinazofanywa na Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO na jeshi la serikali ya DRC, zimepongezwa na viongozi wa dini pamoja na wananchi wa mji wa Mutwanga ulioko katika eneo la Rwenzori jimboni Kivu Kaskazini.