Tanzania yawa mwenyeji wa mafunzo ya wakufunzi wa ulinzi wa amani
Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani Tanzania (TPTC), kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa (UN) kimezindua rasmi mafunzo ya ukufunzi kwa wanadhimu wa Umoja wa Mataifa. Mafunzo hayo yameanza tarehe 7 hadi 18 mwezi huu wa Julai katika chuo hicho kilichoko Dar es Salaam, nchini Tanzania.