Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Dar es salaam

World Bank / Sarah Farhat

Tanzania imepiga hatua katika kuhakikisha kila mtoto anaandikishwa shuleni japo changamoto zipo

Stella Vuzo wa UNIC Dar es Salaam anamuhoji Ayubu Kafyulilo mtaalamu katika shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Tanzania anayesimamia masuala ya ujifunzaji na elimu kwa ajili ya vijana na watoto ambao wako katika mazingira magumu na walio nje ya shule. Kwanza anaanza kwa kueleza hali ya elimu ikoje nchini humo baada ya kuanza kwa mfumo wa elimu bila malipo kwa ngazi ya kuanzia elimu ya awali, msingi hadi kidato cha nne.

Sauti
6'37"
UN News/ Jonatha Joram

Ninarejeleza bidhaa chakavu ili kusafisha mazingira na kuokoa viumbe hai-Jonatha Joram

Ikiwa imesalia takribani miaka kumi kufikia mwaka 2030 ambao umepangwa kuwa mwaka ambao malengo 17 ya maendeleo endelevu, SDGs yatakuwa yametimizwa. Juhudi kote duniani zinaendelea kuhakikisha lengo hilo linafikiwa. Nchini Tanzania, msichana mbunifu Jonatha Joram anayeishi katika jiji la Dar es Salaam ameamua kushiriki katika utunzaji wa mazingira kwa kurejeleza bidhaa ambazo tayari zimetumika ili ziweze kutumika tena badala ya kutupwa na kuchafua mazingira. Katika mahojiano haya na Anold Kayanda wa UN News, Jonatha anaanza kwa kueleza anavyozifanya shughuli zake

Sauti
3'37"
Benki ya Dunia/Screenshot

Mradi wa Benki ya Dunia kusaidia Dar es salaam kukabiliana na mafuriko

Kufuatia mafuriko ya mara kwa mara kwenye jiji la Dar es salaam nchini Tanzania, Benki ya Dunia imedhamini mradi wa kuwezesha wataalamu kutumia mbinu za kisayansi za kuchambua udongo ili kukabiliana na mafuriko. Taarifa zaidi na Amina Hassan. 

Nchini Tanzania katika jiji la Dar es salaam, mmomonyoko wa udongo ni moja ya visababishi vikubwa vya mafuriko ambayo yamekuwa si tu chanzo cha vifo bali pia huharibu miundombinu.

Sauti
2'11"
Picha: IFAD/GMB Akash

Kijana na ajira nchini Tanzania

Nchini Tanzania kijana Richard Hamisi baada ya kuhitimu shahada yake ya biashara na fedha katika Chuo Kikuu Mzumbe, mwaka jana wa 2018, ameandika wazo la kuanzisha maghala ya kutunzia nafaka katika maeneo yanayozalisha mazao mengi nchini huko kama njia mojawapo ya kuhakikisha mazao yanatunzwa vyema na hivyo uhakika wa chakula na bei nzuri  ya mazao. Akihojiwa na Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili  ya Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam, Richard amefafanua kuhusu maghala hayo na kwanza anaanza kwa kueleza alivyopata wazo la kuanzisha mradi huu.

Sauti
2'9"
Benki ya Dunia/Screenshot

Mradi wa Benki ya Dunia kuleta matumaini bonde la Msimbazi Dar es salaam

Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia wanatekeleza  mradi wa kupunguza madhara ya mafuriko kwenye bonde la Msimbazi jijini Dar es salaam, mafuriko ambayo mapema mwaka huu yalisababisha vifo vya watu 15. 

Jiji la Dar es salaam, nchini Tanzania ambalo takwimu zinaonyesha kuwa kutokana na fursa za uchumi zilizopo, kila siku watu 1000 huingia jijini humo.

Sauti
1'34"

Jiji la Dar es salaam lapendeza shukrani kwa UM

Ikiwa leo ni siku ya miji duniani, Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa imeangazia ni kwa jinsi gani chombo hiki chenye wanachama 193 kinasaidia nchi wanachama kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs hususan lengo namba 11 la miji endelevu na jamii. Hatua hiyo inazingatia kwamba kasi ya ukuaji wa miji ni kubwa huku huduma za kijamii zikikua katika kasi ndogo.

Sauti
4'42"