Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza laridhia disemba 12 kuwa siku ya upatikanaji kwa huduma za afya

Mama na mtoto katika kituo cha afya nchini Sudan Kusini. Picha: UM/Video capture

Baraza laridhia disemba 12 kuwa siku ya upatikanaji kwa huduma za afya

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo limeridhia tarehe 12 mwezi disemba kila mwaka kuwa siku ya upatikanaji wa afya kwa watu wote duniani.

Wajumbe wa baraza hilo wamefikia hatua hiyo baada ya kupitisha azimio nambari A/72/L.27 ambalo likipatiwa jina upatikanaji huduma kwa afya ya wote na liliwasilishwa na mwakilishi wa kudumu wa Thailand kwenye Umoja wa Mataifa Balozi  Virachai Plasai ambaye nchi yake ni moja ya wadhamini.

Kwa mujibu wa azimio hilo, mambo yaliyozingatiwa kupitisha siku hii ni kwamba sekta ya afya ni mtambuka na ni jukumu la msingi la kila nchi kupatia wananchi wake.

Kwa manatiki hiyo azimio linakaribisha nchi wanachama, mashirika ya kiraia, sekta binafsi, wasomi na watu binafsi kutambua siku hiyo na kuweka vipaumbele vya afya kwa kuzingatia vigezo mbali mbali kiwemo ajenda ya mwaka 2030 ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ambapo Balozi Plasai amesema..

(Sauti ya balozi Virachai Plasai)

« Pamoja na kuhamasisha uwepo wa mfumo wa afya wenye mnepo na unaorahisisha upatikanaji wa huduma, azimio pia linawekea msisitizo umuhimu wa upatikanaji wa huduma za afya pamoja na dawa na chanjo bora kwa ufanisi na kwa urahisi kwa wote »