Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa, WHO na kundi la wataalam washauri wa chanjo katika ukanda wa Afrika, RITAG, wametoa wito kwa nchi na wadau wa afya kutanguliza huduma za chanjo ambazo zimevurugwa na janga la COVID-19 ili kulinda watoto na jamii dhidi ya magonjwa yanayoweza kuzuiliwa na chanjo.