WHO yaweka vipaumbele muhimu vya utafiti wa afya bora ya wakimbizi na wahamiaji
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO leo jijini Geneva, nchini Uswisi limechapisha ripoti yake ya kwanza kabisa kuhusu ajenda ya utafiti wa Kimataifa ya afya na uhamiaji. Ripoti hii inalenga kuongoza juhudi za utafiti na uelewa na bila shaka kushughulikia mahitaji ya kiafya ya wahamiaji, wakimbizi, na wote waliohamishwa kwa lazima.