Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA
Lugha ya kiswahili kuadhimishwa kimataifa kila tarehe 7 Julai - UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO tarehe 23 mwezi Novemba mwaka 2021 lilitangaza rasmi tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.

Maudhui ya maadhimisho ya mwaka huu ni Kiswahili kwa amani na ustawi. Lengo hasa la maadhimisho haya ya mwaka ni kusongesha matumizi ya lugha ya kiswahili kama nguzo ya amani, na ustawi na wakati huo kuimarisha tamaduni mbalimbali.

UNESCO ilipitisha uamuzi huo huko makao makuu yake mjini Paris Ufaransa wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa shirika hilo.
Azimio lilipitishwa bila kupingwa na utekelezaji wake unaanza mwaka huu wa 2022.

Kupitia ukurasa huu mahsusi, utapataa taarifa zote kuanzia kupitishwa kwa azimio hilo, mapokeo yake na harakati za kukuza lugha ya Kiswahili ili iweze kujenga amani, uchumi, maendeleo na utangamano katika kona mbali mbali za dunia.

Utapata taarifa zilizochapishwa, video kutoka watu mbalimbali iwe maafisa wa serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, maafisa wa UN wenyewe, wanazuoni, wanafunzi na wananchi wa kawaida.


 

UN

Kiswahili sasa kifundishwe vizuri shuleni

Tukigeukia sasa siku ya Lugha ya Kiswahili duniani itakayoadhimishwa Alhamisi ya wiki ijayo Julai 7 mmoja wa wakaazi wa Chukwani Zanzibar Ali Yusuf Mwarabu anasema hatua ya lugha hiyo kutambulika kimataifa kwanza ni Fahari kubwa kwa Wazanzibari lakini pia itakuwa ni fursa nzuri kwa wageni wanaoipenda kujifunza kwa urahisi kuanzia waliko na hata kufunga safari kwenda kisiwani humo.

Sauti
1'35"

01 Julai 2022

Hii leo jarida limejikita katika suala la Kiswahili kuwa lugha ya kimataifa na kuelekea kilele cha maadhimisho tarehe 7 Julai mwaka huu wa 2022. Utasikia mkazi wa Zanzibar akitoa maoni yake, halikadhalika mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda na kisha mashinani mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi. Lakini kumbuka mkutano wa Bahari umefunga pazia hii leo huko Lisbon, Ureno na aliyemwakilisha Katibu Mkuu amesema kile kitakachofuatia, changamoto na fursa. Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.

Sauti
9'58"
UN

Neno la Wiki - Msagaliwa

Hii leo katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunakwenda nchini Tanzania katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA ambako Mhariri Mwandamizi Onni Sigalla anafafanua maana ya neno Msagaliwa.

Anasema huyu ni mwanaume au mvulana ambaye anapenda zaidi kuwa na wanawake muda mwingi au muda wowote. Anasema si ugonjwa bali inatokana na malezi au tatizo la kisaikolojia anapenda kuzungumza na watu wa jinsia nyingine. Wingi wake ni wasagaliwa. Msikilize kwa kina zaidi.

Sauti
59"

30 JUNI 2022

Hii leo jaridani Assumpta Massoi pamoja na Habari kwa ufupi kuhusu Ndui ya Nyani au Monkeypox anamulika pia kiswahili nchini Burundi. Je wafahamu miiko iliyokwamisha kiswahili kuchanua nchini Burundi? Basi Doretee Nshimimana, Mwalimu wa Kwanza wa kiswahili kwenye Vyuo Vikuu Burundi amezungumza na Edouige Emerusenge wa televisheni washirika Mashariki TV na kutanabaisha. Na katika Kiswahili tunafahamishwa maana ya neno, Msagaliwa !! Karibu!

Sauti
12'20"