Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Je Kiswahili sasa kuwa lugha ya kufundishia Tanzania baada ya kukubalika kimataifa?

Je Kiswahili sasa kuwa lugha ya kufundishia Tanzania baada ya kukubalika kimataifa?

Pakua

 

Kuanzia Julai 7 mwaka huu lugha ya Kiswahili sasa itakuwa rasmi lugha ya kimataifa baada ya kutangazwa Novemba mwaka jana na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO kuwa limepitishwa azimio la kuifanya lugha hiyo adhimu na pekee kutoka Afrika kujumuishwa kwenye orodha ya lugha za kimataifa ya shirika hilo. Hii ni hatua kubwa na muhimu hususan kwa mataifa wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili ikiwemo Tanzania ambako inaaminika kuwa ndio chimbuko la lugha hiyo. Na sasa kukubalika kwa Kiswahili kimataifa kutabadili mwelekeo wa sekta muhimu ya elimu nchini humo ambayo kwa kiasi kikubwa inatumia lugha ya Kiingereza kufundishia na kufanya Kiswahili kuwa lugha rasmi ya kufundishia ? Stella Vuzo afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa UNIC Dar es salaam nchini Tanzania amemuuliza swali hilo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anayefafanua kwa kina katika makala hii 

Audio Credit
Anold Kayanda/Samia Suluhu Hassan
Audio Duration
4'11"
Photo Credit
UN Video