UN yamkumbuka Annan, amwagiwa sifa lukuki
Umoja wa Mataifa leo umekuwa na kumbukumbu maalum ya Katibu Mkuu wa 7 wa chombo hicho aliyefariki dunia mwezi uliopita akiwa na umri wa miaka 80.
Umoja wa Mataifa leo umekuwa na kumbukumbu maalum ya Katibu Mkuu wa 7 wa chombo hicho aliyefariki dunia mwezi uliopita akiwa na umri wa miaka 80.
Kwa mara ya kwanza nilivaa viatu baada ya kutoka jandoni, ni kauli ya Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete aliyotoa wakati akizungumzia kilichomo kwenye kitabu chake Safari yangu kutoka mwanafunzi aliyekwenda shule peku hadi Urais, kitabu kitakachozinduliwa hivi karibuni.
Rais wa mkutano wa 73 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ulioanza rasmi hii leo Maria Fernanda Espinosa ametaja mambo muhimu yatakayoongoza utendaji wake kwa kipindi kizima cha mwaka mmoja.
Tangu kifo cha Kofi Annan, nimekuwa nikitafakari ni kitu gani kilimfanya awe wa kipekee! Hivi ndivyo ambavyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewaeleza maelfu ya waombolezaji katika mazishi ya mmoja wa watangulizi wake Kofi Annan aliyezikwa leo huko Accra nchini Ghana. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.
Mabadiliko ya tabia nchi sio ndoto wala kiini macho ni dhahiri, tusipochukua hatua sasa mustakabali wa dunia kwa kizazi hiki na vijavyo uko mashakani , ameonya leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihimiza mshikamano wa kimataifa kuhusu suala hili.
Kikosi maalumu kilichoanzishwa na Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kwa ajili ya kufurusha makundi ya waasi na kujibu mashambulizi (FIB) kinakabiliwa na changamoto nyingi, japo imani ipo kwamba Umoja wa Mataifa utazitatua.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, limetoa ombi la dola milioni 41.7 ili kushughulikia mahitaji ya elimu kwa watoto walioathiriwa na mzozo katika eneo la Ziwa Chad.
Mwaka mmoja tangu warohingya waanze kukimbia jimbo la Rakhine nchini Myanmar kutokana na mateso dhidi yao, bado Umoja wa Mataifa unashindwa kufikisha ipasavyo misaada ya kibinadamu kwa waliosalia jimboni humo.
Hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika kumbukizi maalum ya Katibu Mkuu wa saba wa chombo hicho, Kofi Annan aliyefariki dunia tarehe 18 mwezi huu wa Agosti huko Uswisi baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Leo ni maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kumbukizi na kutoa heshima kwa wahanga wa ugaidi duniani, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ni fursa ya kusikiliza sauti zao pamoja na waathirika wa vitendo hivyo kama njia ya kufanikisha vita dhidi ya ugaidi duniani.