Tulipokuwa na shida Kenya, Kofi alikuwa nasi hadi suluhu kupatikana- Balozi Macharia

22 Agosti 2018

Hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika kumbukizi maalum ya Katibu Mkuu wa saba wa chombo hicho, Kofi Annan aliyefariki dunia tarehe 18 mwezi huu wa Agosti huko Uswisi baada  ya kuugua kwa muda mfupi. 

Katika eneo maalum lililopatiwa jina dirisha la amani ambako watu huenda kwa ajili  ya tafakuri na ibada, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anaungana na wafanyakazi wengine pamoja na mwakilishi wa kudumu wa Ghana kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Martha Ama Akyaa Pobee, kuweka saini kitabu cha kumbukumbu na kuweka shada la maua…

Lengo ni kumkumbuka mwendazake Kofi Annan ambaye alianza kazi Umoja wa Mataifa katika ngazi ya chini hadi akakwea na kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu kuanzia 1997 hadi 2006.

Kisha Antonio Guterres akasema..

“Katika zama za sasa za mgawanyiko mkubwa wa kisiasa na mizozo isiyoisha, tunahitaji azma ya kujenga amani kama ya Kofi Annan kuliko wakati wowote ule.”

 

 Balozi Macharia Kamau wa Kenya.(Picha:UM/Mark Garten)
UN /Mark Garten
Balozi Macharia Kamau wa Kenya.(Picha:UM/Mark Garten)

Je kwa waliowahi kufanya naye kazi wanasemaje? Balozi Macharia Kamau, Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya nje ya Kenya ambaye amewahi kuwakilisha nchi yake kwenye Umoja wa Mataifa akizungumza na UN News  ameelezea mengi kuhusu mwendazake Kofi Annan na pia kwanini wakenya wanamkumbuka sana.

 

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter