Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihudhuria mkutano wa sayansi,teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM) kuhusu programu za kompyuta.
UN Photo/Antonio Fiorente

Wanasayansi wasichana wa Afrika wako mstari wa mbele katika vita ya kuleta usawa wa kijinsia katika sayansi-Antonio Guterres.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo hii mjini Addis Ababa Ethiopia amekutana na kuzungumza na wasichana kutoka nchi mbalimbali barani Afrika ambao wanashiriki katika mpango wa kuwafanya kubobea katika programu za kompyuta, mkakati wa unaoratibiwa kwa pamoja kati ya Muungano wa kimataifa wa Mawasilino (ITU) na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya wanawake UN Women.

kamishina mkuu UNHCR Filipo Grandi
Arthur Max/FM. Ministério das Relações Exteriores

UNHCR yaomba radhi kwa Tanzania kutokana na sakata la nguo za msaada kwa wakimbizi zilizofanana na sare za kijeshi.

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, Filipo Grandi akiwa ziarani nchini Tanzania  amesema Tanzania kwa muda mrefu imekuwa ni karimu hususan kwa wakimbizi ambao wanakimbia machafuko na rais wake John Magufuli amerejelea kuwa ukarimu huo hautafika mwisho.

 

Sauti
2'17"
Wajumbe wa Baraza la Usalama walipokutana Januari 26 2019 kujadili hali ilivyo Venezuela
UN /Manuel Elias

 Venezuela barazani, wajumbe wavutana iwapo ni tishio kwa usalama duniani au la!

Vuta nikuvute kuhusu hali inayoendelea nchini Venezuela kwa sasa, imedhihirika leo kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo lilikutana kwenye kikao cha dharura kujadili kinachoendelea wakati huu ambapo  kuna mvutano kati ya Rais Nicolas Maduros wa  nchi hiyo na Juan Guido rais wa Bunge ambaye amejitangaza rais wa muda wa Venezuela.