Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akizungumza na wanahabari katika mpaka wa Rafah, Misri.
UN Photo/Mark Garten

Guterres: Ni wakati wa Gaza kufurika misaada ya kibinadamu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amewaambia waandishi wa habari katika mpaka wa Rafah unaovuka kuingia Ukanda wa Gaza kwamba ni wakati wa kusitishwa kwa mapigano na kwa "dhamira ya kidhalimu ya Israel" kuruhusu uwasilishaji wa misaada bila vikwazo katika eneo la Palestina lililozingirwa alipokuwa akianza safari yake ya kila mwaka ya mshikamano wakati wa mwezi wa  Ramadhani siku ya Jumamosi, ziaranatakayozuri nchi za Misri na Jordan.

 

 

Watoto wa Kipalestina wa Ukanda wa Gaza wakiwa na taa kusherehekea mwezi tukufu wa Ramadhani.
© UNRWA

Mkuu wa UN aanza ziara ya mshikamano kipindi cha Ramadani huko Misri na Jordan

Kutokana na kuongezeka kwa mizozo na migogoro ya kibinadamu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameanza safari yake ya kila mwaka ya mshikamano kipindi cha Ramadhani, inayoanza wikendi hii mjini Cairo, Misri. Safari hiyo ambayo inasadifiana na mwezi mtukufu wa Ramadhani, inafanyika katika nyakati za misukosuko hasa kutokana na mzozo unaoendelea huko Gaza.

wasichana wakimbizi wa ndani katika kituo kinachosaidiwa na UNICEF cha Al Salam Sudan
© UNICEF/Ahmed Elfatih Mohamdeen

Usafirishaji binadamu kwa ajili ya biashara ya ngono na utumiaji watoto vitani vyaongezeka Sudan: Wataalam UN

Wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa leo wameelezea wasiwasi wao kuhusu kuongezeka kwa ripoti za ulanguzi wa binadamu hasa wanawake na wasichana, kwa madhumuni ya unyanyasaji wa kingono na utumwa wa kingono, ndoa za utotoni na za kulazimishwa, na kuajiri wavulana kushiriki katika mapigano nchini Sudan, kutokana na kuendelea kuzorota kwa mgogoro wa kibinadamu nchini humo ambao umesababisha watu zaidi ya milioni 9 kufungasha virago na kuyahama makazi yao.

Vassily Nebenzia, Mwakilishi wa Kudumu wa Urusi katika kura za Umoja wa Mataifa dhidi ya rasimu ya azimio wakati wa mkutano kuhusu hali ya Mashariki ya Kati, ikiwa ni pamoja na suala la Palestina.
UN Photo

Kura mbili za turufu zaipinga rasimu ya azimio la Marekani la “umuhimu mkubwa” kusitisha mapigano Gaza

Katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililokaa asubuhi hii ya Machi 22 saa za New York Marekani, Urusi na China zimepinga kwa kura ya turufu rasimu ya azimio la Marekani lililotaka "ulazima" kwa usitishaji mapigano haraka na thabiti "kuwalinda raia kutoka pande zote," kuwezesha uwasilishaji wa misaada inayohitajika na kuunga mkono mazungumzo yanayoendelea kati ya Israeli na Hamas.

Watu waliokimbia makazi yao kutokana na migogoro wanaishi katika kambi ya muda karibu na Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
© WFP/Benjamin Anguandia

Mlipuko wajeruhi watoto wanne Minova nchini DRC, UNICEF yaonya uwezekano wa madhila zaidi

Ongezeko kubwa la ghasia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambalo limesababisha takriban watu 400,000 kupoteza makazi katika Kivu Kaskazini tangu mwanzoni mwa mwaka kuna hatari ya kuwaweka watoto kwenye ghasia zaidi kama ulinzi wao hauwezi kuimarishwa, limeonya leo Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudmia watoto (UNICEF).