Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu wa UN alaani shambulio la kigaidi nchini Urusi

Muonekano wa mji wa Moscow, Urusi
UN Photo/Paulo Filgueiras
Muonekano wa mji wa Moscow, Urusi

Katibu Mkuu wa UN alaani shambulio la kigaidi nchini Urusi

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali shambulio la kigaidi lililotekelezwa leo kwenye ukumbi wa tamasha nje ya mji wa Moscow, nchini Urusi ambapo takriban watu 40 wameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa leo jioni kwa saa za New York Marekani Katibu Mkuu Guterres ametuma salamu za rambirambi kwa familia zilizofiwa, wananchi pamoja na Serikali ya  Urusi.

Pia amewatakia majeruhi wote ahueni ya haraka.