FAO Kenya na wadau wathibitisha ulemavu sio kulemaa
Stephen Omondi Odhiambo kwa kutumia lugha ya ishara anasema neno “KUKU” kwa mkewe, Dorah Akungu, na mara moja mkewe anaelewa. Kwa maneno ya ishara za vidole, Stephen amemfundisha mkewe, familia yake na marafiki wa karibu ishara za maneno yanayotumiwa sana na sasa wanawasiliana kwa urahisi.