Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhusiano wa kijamii huondoa upweke na kuboresha afya kwa jamii – WHO

Maria Ondosia Mawero, mama mzee kutoka Kenya ambaye ameishi maisha ya upweke kwa muda mrefu. Sasa anasikiliza mahubiri na muziki wa kanisa kupitia redio na mara nyingi hukutana na marafiki ili kupunguza upweke.
WHO

Afya

Mwezi Novemba mwaka jana shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO lilizindua Kamisheni  ya kuchochea Muunganisho wa Kijamii au Social Connection kwa lengo la kuondokana na tatizo la upweke ambalo limetambuliwa kuwa moja ya tishio kubwa la afya duniani. WHO inasema kutengwa na jamii na kuishi maisha ya upweke ni jambo hatari, chungu, na zaidi hatari kwa afya ya binadamu.

Upweke  unaweza kuathiri mtu yeyote, wa hali yeyote mahali popote. Kamisheni hiyo sasa kupitia video za Muunganisho wa Kijamii hufikia watu kote ulimwenguni wanaoishi pekee yao lengo kuu likiwa ni kuwapatanisha na kuwashirikisha na jamii pamoja na marafiki ili waondokane na msongo wa mawazo na kuboresha afya yao. 

Maria Ondosia Mawero, mama mzee kutoka Kenya ambaye ameishi maisha ya upweke kwa muda mrefu. Sasa anasikiliza mahubiri na muziki wa kanisa kupitia redio na mara nyingi hukutana na marafiki ili kupunguza upweke.
WHO
Maria Ondosia Mawero, mama mzee kutoka Kenya ambaye ameishi maisha ya upweke kwa muda mrefu. Sasa anasikiliza mahubiri na muziki wa kanisa kupitia redio na mara nyingi hukutana na marafiki ili kupunguza upweke.

Tayari msusururu wa video hizo umeanza kuchapishwa mitandaoni ambapo tunakutana na Maria Ondosia Mawero, mama mzee anayeishi katika eneo la mabanda la Kibera jijini Nairobi, nchini Kenya akitueleza ni kwa nini uhusiano wa kijamii ni muhimu kwa afya yetu, ustawi na ubinadamu wetu. Yeye ameishi maisha ya upweke kwa muda mrefu na anasema,  

“Maisha sasa yananielemea hapa. Mume wangu alipofariki, watoto wangu pia walimfuata. Natamani Mungu angeniacha na mtoto hata mmoja. Hilo lingeituliza nafsi yangu nikisikia tu naitwa mama.” 

Msongo wa mawazo umeathiri watu wengi hususani wale ambao mara nyingi wanaishi pekee yao. Kwa María kando na upweke, changamoto zitokanayo na uzee unaongeza machungu, Maria anaongeza kuwa, “Ninapofikiria shida zote nilizo nazo, ninajisikia vibaya sana. Ninachopitia sasa ni mateso chungu mzima. Sina chochote.” 

Maisha ya Maria yameathiriwa vibaya kutokana na kutengwa na jamii yake na sasa anaishi peke yake. Akijikongoja nje ya kibanda anamoishi hapa Kibera machungu ni dhahiri usoni mwake.

“Unapotembea mitaani watu wanakuona tu na kusema hufai. Nikikutana na mtu ambaye anataka kunisaidia, machozi yangu yanaanza kutiririka nikisema tu asante sana.” 

Licha ya changamoto hizo, Maria anatoa ushauri kwa watu ambao wamejikuta wakiishi pekee yao kama yeye, “Ni muhimu kutojitenga na kuishi pekee yako. Nenda kwa marafiki zako, nenda kanisani, sikiliza mahubiri na utahisi moyo wako ukitoka kwenye huzuni.”  

Maria Ondosia Mawero, mama mzee kutoka Kenya ambaye ameishi maisha ya upweke kwa muda mrefu. Sasa anasikiliza mahubiri na muziki wa kanisa kupitia redio na mara nyingi hukutana na marafiki ili kupunguza upweke.
WHO
Maria Ondosia Mawero, mama mzee kutoka Kenya ambaye ameishi maisha ya upweke kwa muda mrefu. Sasa anasikiliza mahubiri na muziki wa kanisa kupitia redio na mara nyingi hukutana na marafiki ili kupunguza upweke.

Ili kuondokana na upweke, Maria amepata kusudi katika kulea paka wanaozurura mitaani na pia hutumia hushiriki mikutano na marafiki. 

“Nikifikiria jinsi nilivyojihisi nilipokuwa pekee yangu na sikushiriki vikundi vyovyote vya watu, nilihisi tofauti nilipoanza kujiunga na vikukundi. Niligundua kuwa nilipokuwa peke yangu, kwamba nilikuwa na msongo wa mawazo na huzuni ambayo yalinishika na nilinaswa na mawazo yangu. Kuishi kunamaanisha kuishi kwa upendo na amani na watu. Sasa una amani na roho yako.” 

Upweke unaweza kuathiri mtu yeyote, mahali popote, iwe ni watoto, vijana, wazee, wanawake au wanaume. Shukrani sana kwa WHO, kwa kuchochea uhusiano wa kijamii kupitia vipindi vya muungano wa kijamii ambavyo vimesaidia Maria na wengine ambao wamefuatilia video zao. Hakika nguvu za upatanisho zinaweza kuleta mabadiliko chanya na afya bora kwa jamii.