Hatari ya kutetea wanawake wanaotuhumiwa kwa uchawi nchini Papua New Guinea
Nchini Papua New Guinea, suala la kuwatetea wanawake wanaotuhumiwa kwa uchawi, imekuwa kazi ya kutishia maisha.
Nchini Papua New Guinea, suala la kuwatetea wanawake wanaotuhumiwa kwa uchawi, imekuwa kazi ya kutishia maisha.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC sasa imejiunga rasmi na Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuwa mwanachama wa saba. Rais wa DRC Tshisekedi aliye ziarani Kenya kwa siku mbili ametia rasmi saini mkataba wa uanachama.
Shrikia la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limesema Pembe ya Afrika inakabiliwa na ukame mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miongo kadhaa hali ya ukame, kuongezeka kwa uhaba wa chakula na kusababisha watu wengi kuhama makazi yao.
Umoja wa Mataifa leo umelaani vikali shambulio lililotekea kwenye stesheni ya treni ya Kramatorsk Kaskazini mwa jimbo la Donetsk nchini Ukraine linalodaiwa kukatili maisha ya raia 39 miongoni mwao ni watoto na kujeruhi wengine wengi waliwemo waliojeruhiwa vibaya sana.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema vita nchini Ukraine vimesababisha moja ya ongezeko kubwa kabisa na la haraka la watu kutawanywa na janga la kibinadamu kuwahi kutokea.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Catherine Russell ametoa wito wa azimio la haraka la kisiasa ili kukomesha ghasia zinazoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.
Tathimini ya utafiti wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO umebaini kwamba hadi asilimia 65% ya Waafrika wameambukizwa SARS-CoV-2, virusi vinavyosababisha COVID-19.
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa , leo limepiga kura kupitisha azimio linalotaka Urusi isitishe uanachama kwenye Baraza la Haki za binadamu .
Debies Joseph mshindi namba tatu katika mashindano ya tuzo ya ujasiliamali mdogo ya wachakataji wa dagaa kutoka katika nchi kumi na tano ulimwenguni chini ya shirika la women in see food industry, ameweza kutimiza lengo namba moja la maendeleo endelevu ya umoja wa mataifa linalohimiza kutokomeza umaskini.
Walinda amani wa kikosi cha 5 cha Tanzania, TANBATT 5 kinachohudumu katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa unaolinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA, wamewatembelea na kuwapelekea zawadi balimbali yakiwemo mavazi, wafungwa wanawake katika gereza la Berberati, mkoa wa Mambelekadei.