Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Walinda amani wanahamasisha jamii kufanya shughuli za maendeleo kwa ajili ya nchi yao ya Jamhuri ya Afrika ya Kati

Walinda amani wa TANBATT 5 watoa misaada kwa wanawake gerezani, Berberati, CAR

© MINUSCA/ Ipo Souare Mabongo
Walinda amani wanahamasisha jamii kufanya shughuli za maendeleo kwa ajili ya nchi yao ya Jamhuri ya Afrika ya Kati

Walinda amani wa TANBATT 5 watoa misaada kwa wanawake gerezani, Berberati, CAR

Msaada wa Kibinadamu

Walinda amani wa kikosi cha 5 cha Tanzania, TANBATT 5 kinachohudumu katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa unaolinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA, wamewatembelea na kuwapelekea zawadi balimbali yakiwemo mavazi, wafungwa wanawake katika gereza la Berberati, mkoa wa Mambelekadei.

Nathaniel Simon, ni Mshauri wa masuala ya kijinsia wa MINUSCA katika ukanda wa magharibi anasema, “kwa furaha ninapenda kuchukua nafasi na kusema kuwa tumeungana siku ya leo kuonesha nafasi ya mwanamke katika jamii. TANBAT na MINUSCA tunaheshimu haki za binadamu.”  

Bi. Simon anendelea kueleza kuwa MINUSCA kwa kushirikiana na wizara ya haki ya Jamhuri ya Afrika ya Kati wanaendelea kunajitahidi kuboresha maisha ya ndani ya gereza hili akisema, “neno langu kuu ni umuhimu wa mwanamke katika jamii ya Afrika ya Kati na kuendelea kuheshimu haki za mwanamke popote alipo hata waliofungwa bado ni wanawake wanaohitaji kutendewa haki.” 

Kwa upande wake Rais wa gereza hilo Bwana Wankian Mamase akasema ana neno la shukrani kwa walinda amani kutoka Tanzania yaani TANBAT 5 na kwa Umoja wa Mataifa kupitia MINUSCA.  

“Kwa niaba ya wafungwa wanawake na nyumba ya sheria Berberati napenda kuwashukuru MINUSCA kupitia TANBAT kwa kuweza kusaidia kuweka mazingira salama katika eneo letu kijamii bila kusahau haki za binadamu na wanawake kwa ujumla. Mmeonesha kwa jinsi gani mnathamini haki za binadamu kwa kujitoa kwenu kushiriki na wanawake waliopo hapa gerezani. Napenda kutoa wito kwa wanawake waliotembelewa leo hapa gerezani watumie mchango waliopewa na TANBAT kujitafakari ili kuweza kuepukana na changamoto zinazoweza kuwaweka kizuizini.”