Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Soko la Samaki Mwanza Tanzania

Dola moja yamuondoa mwanamke mjasiriamli katika mstari wa umaskini

UN News
Soko la Samaki Mwanza Tanzania

Dola moja yamuondoa mwanamke mjasiriamli katika mstari wa umaskini

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Debies Joseph mshindi namba tatu katika mashindano ya tuzo ya ujasiliamali mdogo ya wachakataji wa dagaa kutoka katika nchi kumi na tano ulimwenguni chini ya shirika la women in see food industry, ameweza kutimiza lengo namba moja la maendeleo endelevu ya umoja wa mataifa linalohimiza kutokomeza umaskini.

Umoja wa Mataifa umekuwa ukihamasisha serikali, mashirika ya kimataifa na asasi za kiraia kuchukua jukumu la kutekeleza malengo 17 ya maendeleo endelevu SDGs ili jamii yote uweze kunufaika na malengo hayo ambayo yanalenga kuinua wananchi katika kila nyanja ya maisha. 

Wito huo umekuwa ukiitikiwa na wadau mbalimbali na matokeo chanja yamekuwa yakionekana mathalani nchini Tanzania katika mkoa wa Mwanza ambapo Debies Joseph mshindi namba tatu katika mashindano ya tuzo ya ujasiliamali mdogo ya wachakataji wa dagaa kutoka katika nchi kumi na tano ulimwenguni chini ya shirika la women in see food industry, ameweza kutimiza lengo namba moja la maendeleo endelevu ya umoja wa mataifa linalohimiza kutokomeza umaskini.

Katika mahojiano maalumu na Evarist Mapesa wa Radio washirika Radio SAUT FM ya jijini mwanza Tanzania,Debies anasema alianza biashara yake akiwa na mtaji wa dola moja sawa na shilingi elfu tatu lakini sasa amekuza mtaji wake mpaka kufikia dola 130.

“nilianza kujihusisha na hii biashara ya kukaanga dagaa na samaki kwasababu nilikuwa nimekaa tu nyumbani bila kazi ya kufanya,nikaona ni bora nitafute biashara ya kufanya ili kukidhi mahitaji ya watoto wangu na nilianza kwa mtaji wa shilingi elfu tatu lakini sasa mtaji wangu umekuwa hadi kufikia shilingi laki tatu na elfu hamsini”,alisema Debies
Mwanza ni mkoa ambao umezungukwa na ziwa Victoria ambalo wavuvi hulitumia kuvua samaki na dagaa ili kuwawezesha kupata mahitaji yao ya kila siku.

Debies aliamua kuitumia ipasavyo fursa ya upatikanaji wa dagaa na samaki katika eneo hilo ili aweze kusimama kiuchumi na kusaidia familia yake kupata mahitaji bila utegemezi kutoka kwa ndugu,jamaa na marafiki licha ya kuanza na mtaji mdogo.
“nilivyoanza biashara ilikuwa ndogo sana,hiyo shilingi elfu tatu niliigawanya kwa kununua mafuta, kuni na samaki,kadri siku zilivyoenda ndivyo mtaji wangu ulikuwa unazidi kukua kila siku na sasa ninachukua ndoo saba hadi nane za dagaaa kila siku ”alisema Debies.

Biashara hii imemsaidia kusomesha watoto wake hadi vyuo vikuu, vyuo vya kati nan a kufanikiwa kujenga nyumba nzuri ya kisasa na kumudu kuendesha familia yake bila utegemezi na kuwa na misuli ya kiuchumi.

Wanawake wajasiriamali katika soko la samaki la Luchelele jijini Mwanza Tanzania
UN News
Wanawake wajasiriamali katika soko la samaki la Luchelele jijini Mwanza Tanzania

Debies mkombozi wa familia 

Debies pamoja na familia yake wamekuwa wakiamka majira ya saa kumi na moja alfajiri na kuelekea katika mwalo wa Sweya au jembe ili kukutana na wavuvi wanaowauzia dagaa pamoja na samaki hizo
Familia yake imekuwa ikimsaidia katika hatua mbalimbali za utengenezaji,uchakataji na upakiaji wa dagaa kwenda kwa wateja wake waliopo katika maeneo mbalimbali ya Tanzania.
Naomi Joseph ambaye ni dada yake Debies, anasema kuwa biashara hiyo imewasaidia kuweza kutatua changamoto zao za kifamilia. 

“sisi wana familia biashara yake inatusaidia kwa mahitaji,chakula, amejenga hapa mji na tunaishi vizuri kutokana na biashara yake Debies”,alisema Naomi.

Naomi anasema kuwa kama wanafamilia wamekuwa bega kwa bega na debies ili kuhakikisha kuwa wanamsaidia katika baadhi ya kazi “kila kazi anayoleta tunamsaidia kuosha dagaa,kuzoa  kukaanga na hata kupakia kwenye vifurushi kabla ya kwenda kwa wateja wake”

Changamoto anazokumbana nazo

Mbali na mafanikio hayo ambayo Debies anasema kuwa biashara yake imekuwa ikikutana na changamoto mbalimbali ikiwemo kupanda kwa bei ya mafuta ya kula.

“ugumu upo katika biashara hii mfano kama sasa hivi nakabiliana na changamoto ya mafuta ambapo zamani kabla hayajapanda lita ishirini tulikuwa tunaachukulia kwa shilingi elfu sitini hadi elfu sabini lakini kwa sasa tunauziwa shilingi elf tisini na tano, mafuta yamekuwa bei ya juu,kuni pia bei yake ipo juu na mwaloni pia unachukua mzigo kwa bei kubwa”,alisema debies.

“pili mvua zinapoanza kunyesha ninapata shida,unakuta dagaa hainyauki maji inatubidi tutumie mafuta mengi zaidi” aliongeza Debies.

Licha ya changamoto hizo lakini Debies amekuwa akiendelea kupambana na mikikimikiki hiyo bila kukata tamaa
kwa wengine ambao wanataka fursa kama hizi nini wakifanye?

Mtaalam wa uchumi na mhadhiri mwandamizi wa uchumi kutoka chuo kikuu cha mtakatifu agustino SAUT Dr Isack Safari anasema kuwa fursa zipo katika maeneo mbalimbali ni suala la kuzitambua na kuzichangamkia.

“ni suala la kujiangalia katika maisha yako,na ujitafakari mwenyewe kwanza ujiulize unataka nini, ili uweze kuijua hiyo unataka nini lazima kuwe na tatizo au shida fulani katika eneo lako ,kwa mfano kipato chako sio cha uhakika ungependa upate kipato cha uhakika,sasa utafanyake?hapo ndo unaanza kutafuta fursa zitakazokuwezesha wewe angalau uwe na kipato cha uhakika “,alisema Dr. Safari

“jambo la pili lazima uwe na bidii,kutokukata tamaa, na kujitoa kikamilifu katika hicho kitu unachokitafut kwa ukamilifu,ukiweza kumudu hayo yote utakuwa umeweza kuzichangamkia fursa katika maeneo tunayoishi maana bado katika jamii kuna changamoto ya uhitaji wa vitu Fulani,” alisema Dr.Safari.