Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu zaidi ya milioni 4 sasa ni wakimbizi nje ya Ukraine na milioni 7.1 wametawanywa ndani ya nchi 

Familia ikiwa Kramatorsk kituo cha reli ikisubiri kuondoka kuelekea Kyiv.
© UNICEF/Julia Kochetova
Familia ikiwa Kramatorsk kituo cha reli ikisubiri kuondoka kuelekea Kyiv.

Watu zaidi ya milioni 4 sasa ni wakimbizi nje ya Ukraine na milioni 7.1 wametawanywa ndani ya nchi 

Msaada wa Kibinadamu

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema vita nchini Ukraine vimesababisha moja ya ongezeko kubwa kabisa na la haraka la watu kutawanywa na janga la kibinadamu kuwahi kutokea. 

Shirika hilo linasema ndani ya wiki sita pekee zaidi ya watu milioni 4.3 wamekimbia nchi yao na kuwa wakimbizi huku wngine milioni 7.1 wametawanywa ndani ya Ukraine. 

UNHCR inashirikiana  kwa karibu na mamlaka ndani ya Ukraine ili kuongeza uwezo wa meneo yanayopokea wakimbizi. 

Usambazaji wa misaada bado ni changamoto 

Akizungumza na waandishi wa Habari mjini Geneva Uswis hii leo msemaji wa UNHCR Matthew Saltmarsh amesema kutoa misaada bado ni changamoto katika sehemu za nchi ambako kuna mapigano makali.  

“Tunaendelea kujitahidi kufikia maeneo yaliyoathirika sana kama vile Mariupol na Kherson kwa usaidizi wa kuokoa maisha kama sehemu ya misafara ya mashirika ya misaada ya kibinadamu na tumechangia misafara minne kama hii chini ya mfumo wa taarifa za kibinadamu, miwili kwa eneo la Sumy, mmoja Kharkiv na mmoja Sieverodonetsk, na kusaidia misafara kadhaa ya ziada kwa msaada wa washirika, na  kuweza kufikia watu 15,600 kwa vitu vya misaada.” 

Maksym mwenye umri wa miaka sabab alilazimika kuodoka Mariupol mashariki mwa Ukraine.
© UNICEF
Maksym mwenye umri wa miaka sabab alilazimika kuodoka Mariupol mashariki mwa Ukraine.

Msafara wa hivi karibuni zaidi ulikuwa tarehe 6 Aprili, ambapo UNHCR ilikuwa miongoni mwa wale waliopeleka misaada Sievierodonetsk huko Luhansk, mashariki mwa Ukraine.  

Kwa wiki kadhaa, watu huko wamevumilia kupigwa makombora na uhaba wa vitu vya msingi kama vile maji, gesi na umeme.  

“Timu yetu iliweza kutoa taa za sola,mablanketi, vifaa vya usafi, maziwa ya mtoto na maturubai kwa watu 3,000.” Ameongeza msemaji huyo. 

UNHCR pamoja na washirika wa mashirika yasiyo ya kiserikali inaendelea kutoa huduma za ulinzi na kuwaelekeza wakimbizi kwa kwenda kwa mamlaka katika vituo vya mpakani na vituo vya mapokezi.  

Watu wapatao 36,000 wamepokea usaidizi kama huo na taarifa katika vituo vya mpakani, vya mpito, na vituo vya kupokea wageni na kupitia simu za dharura. Huduma hizi ni pamoja na usaidizi wa kisheria na usaidizi wa kisaikolojia miongoni mwa mambo mengine.  

UNHCR pia hutoa huduma za ulinzi karibu na maeneo yenye mizozo, mara tu wanapowasili.  

Washirika wa UNHCR bado wako na uwezo mkubwa wa ulinzi huko Donetsk na Luhansk, wakati katika maeneo mengine yanayokabiliwa moja kwa moja na uhasama 

UNHCR yapanua wigo wa msaada 

Ili kuwawezesha kutoa kipaumbele kwa mahitaji ya muhimu zaidi kwa wakimbizi, na kutimiza mwitikio unaoongozwa na mamlaka ya kitaifa nchini Poland, UNHCR inapanua wigo wa usaidizi wa pesa taslimu.  

Zaidi ya watu 10,000 wamejiandikisha huko Warsaw kwa muda wa wiki mbili zilizopita.  

UNHCR ilifungua kituo cha pili huko Krakow wiki hii. Maeneo ya ziada ya uandikishaji yanafunguliwa hivi karibuni kwa ushirikiano na mashirika yasiyo ya kiserikali ya serikali na ya kitaifa.