Maeneo ya shule sio sehemu za mapigano: Guterres
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kulinda maeneo ya shule dhidi ya mashambulizi, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekemea tabia ya makundi yanayopigana kuvamia maeneo ya shule, kukamata watu mateka na vikosi vya ulinzi kufanya maeneo ya shule kama sehemu zao za kuweka kambi za mapigano.