Homa ya uti wa mgongo yazuka DRC, watu 129 wameshapoteza maisha:WHO

8 Septemba 2021

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa limesema serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, imetangaza mlipuko wa homa ya uti wa mgomo katika jimbo la Tshop Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo

Mpaka sasa watu 129 wameshafariki dunia na wengine 261 wakishukiwa kuambukizwa ugonjwa huo. 
Taarifa iliyotolewa leo na WHO inasema idadi ya vifo vinavyoripotiwa kutokana na ugonjwa huo ni kubwa ikiwa ni uwiano wa asilimia 50%. 

Vipimo vya uthibitisho vilivyofanywa na taasisi ya Institut Pasteur huko Paris nchi Ufaransa imebaini kuwa ni Neisseria meningitidis moja ya aina vijududu vya Bakteria vinayozuka mara kwa mara na kusababisha mlipuko mkubwa wa homa ya uti wa mgongo  
Mamlaka za afya zimetuma timu ya dharura ya awali, kwenda katika eneo lililoathirika na kwa msaada wa WHO juhudi zinaendelea ili kuharakisha hatua za kudhibiti mlupuko huo.  

Kamati ya kukabiliana na smajanga imeundwa huko Banalia, katika jamii iliyoathiriwa na mlipuko huo, na pia huko Kisangani, mji mkuu wa Tshopo, ili kuharakisha juhudi za kudhibiti mlipuko.  

WHO imetoa vifaa vya matibabu huko Banalia na ina mpango wa kupeleka wataalam zaidi na rasilimali. 

Akizungumzia mlipuko huo Dkt. Matshidiso Moeti, mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika amesema “Homa ya uti wa mgongo ni maambukizo mazito na ni changamoto kubwa kwa afya ya umma. Tunajitahidi kupambana nayo kwa kasi, tunatoa dawa na kupeleka wataalam kuunga mkono juhudi za serikali za kudhibiti mlipuko huo kwa muda mfupi zaidi.”  

Ameongeza kuwa zaidi ya wagonjwa 100 tayari wanapata matibabu nyumbani na katika vituo vya afya huko Banalia. Homa ya uti wa mgongo huambukizwa miongoni mwa watu kupitia mate au makohozi yaliyotemwana watu walioambukizwa. 

Pia kwa karibiana, kuwa karibu kwa muda mrefu au kuishi karibu na mtu aliyeambukizwa kunasaidia kuenea kwa ugonjwa huo.  
Ingawa watu wa kila umri wanaweza kupata ugonjwa huu, huathiri sana Watoto wachana, Watoto wa umri mdogo na vijana. 

 "Tunaongeza hatua za kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo ndani ya jamii na kuchunguza kwa haraka visa vinavyoshukiwa katika maeneo jirani ili kutibu wagonjwa na kupunguza maambukizo yanayoweza kuenea," amesema Dkt. Amédée Prosper Djiguimdé, Mwakilishi wa WHO katika nchini DRC.  

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter