Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utegemezi wa bidhaa kwa ajili ya mauzo ya nje umeongezeka : UNCTAD

Hali ya kutegemea bidhaa kutoka nje imeongezeka maradufu duniani,mbili ya tatu ya nchi zinazoendelea zipo hatarini kiuchumi kutokana na hali hii
World Bank/Thomas Michael Perry
Hali ya kutegemea bidhaa kutoka nje imeongezeka maradufu duniani,mbili ya tatu ya nchi zinazoendelea zipo hatarini kiuchumi kutokana na hali hii

Utegemezi wa bidhaa kwa ajili ya mauzo ya nje umeongezeka : UNCTAD

Ukuaji wa Kiuchumi

Utegemezi wa bidhaa kwa ajili ya mauzo ya nje umeongezeka katika muongo mmoja uliopita kutoka  nchi 93 kuanzia mwaka wa 2008 hadi 2009  na nchi 101 katika  mwaka 2018-2019

Kwa mujibu wa ripoti ya kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD juu ya utegemezi wa bidhaa mwaka 2021 ambayo imetolew leo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya UNCTAD thamani ya mauzo ya bidhaa ulimwenguni ilifikia dola trilioni 4.38 katika 2018-2019, ikiwa ni ongezeko la asilimia 20 ikilinganishwa na mwaka kati ya 2008-2009. 

Akizungumzia ripoti hiyo, mkuu wa kitengo cha bidhaa, UNCTAD Janvier Nkurunziza amesema,"Utegemezi wa bidhaa hufanya nchi kuwa katika hatari zaidi ya mshtuko mbaya wa kiuchumi," Ameongeza kwamba, "Inaweza kuwa na athari mbaya kwa usafirishaji na mapato ya kifedha na kuathiri vibaya maendeleo ya uchumi wa nchi." 

Kulingana na UNCTAD nchi inazingatiwa kuwa tegemezi ya usafirishaji wa bidhaa wakati zaidi ya asilimia 60 ya mauzo yake yote ya bidhaa yanajumuishwa na bidhaa. 

Ripoti pia imetanabaisha kwamba nchi nyingi zilizokuwa zinategemea mauzo ya bidhaa mwaka 2008 hadi 2009 zinasalia hivyo mwaka 2018-2019. 

Halikadhalika utegemezi wa bidhaa kwa kiasi kikubwa unaathiri nchi zinaoendelea huku nchi 87 zikitajwa kuwa tegemezi wa bidhaa mwaka 2018-2019. Kati ya nchi hizo 1010 zinazotegemea bidhaa 2018-2019, 38 zilitegemea bidhaa za kilimo, 32 mauzo ya madini na 31 mafuta. 

UNCTAD unakadiria uchumi kuporomoko kwa dola Trilioni 1 mwaka 2020
UNCTAD/Jan Hoffmann
UNCTAD unakadiria uchumi kuporomoko kwa dola Trilioni 1 mwaka 2020

Utegemezi wa bidhaa umekithiri bara Afrika na Oceania huku ni dhahiri huku robo tatu ya nchi katika kanda hizo mbili zikitegemea mauzo ya bidhaa nje kwa asilimia 70 ya pato la  mauzo ya bidhaa nje. 

Hali ya utegemezi wa bidhaa imekithiri katika Afrika ya Kati na Afrika Magharibi, ambapo ikikadiriwa kuwa  karibu asilimia 95. Katika maeneo hayo mawili mbili, nchi zote zilitegemea  bidhaa katika kipindi cha mwaka 2018-2019, isipokuwa Jamhuri ya Afrika ya Kati. 

Huko Amerika Kusini, nchi zote 12 zilikuwa na kiwango cha utegemezi wa bidhaa zaidi ya asilimia 60 mnamo 2018-2019, na kwa robo tatu yao, sehemu ya mauzo ya bidhaa nje ilizidi 80%. 

Asia ya Kati ilikuwa eneo ambalo lilikuwa na kiwango cha juu cha utegemezi wa bidhaa huko Asia, na wastani wa sehemu ya mauzo ya bidhaa nje ikiwa zaidi ya asilimia 85 mnamo 2018-2019. Nchi zote tano katika eneo hilo zilizingatiwa kuwa tegemezi ya usafirishaji wa bidhaa mnamo 2018-2019. 

Takwimu kuhusu utegemezi wa bidhaa kwa wamuzo ya nje miongoni mwa nchi wanachama wa UNCTAD utachangia katika mazunugmzo ya mkutano wa bidhaa kimataifa utakaofanyika Septemba 13 hadi 15.