Afghanistan: UN inahitaji dola milioni 600 kwa shughuli za kibinadamu

7 Septemba 2021

•    . Dola milioni 600 zahitajika kunusuru maisha Afghanistan
•     Watoto zaidi ya 300 watenganishwa na familia zao
•    Uhakika wa chakula ni mtihani mkubwa

Katika miezi sita ya kwanza ya mwaka 2021, WFP imetoa msaada kwa watu milioni 5.5 nchini Afghanistan. 

Wakati Afghanistan inakabiliwa na "kusambaratika kwa huduma zake za msingi na msaada wa chakula," Umoja wa Mataifa leo Jumanne umeomba zaidi ya dola milioni 600 kufadhili miradi yake ya kibinadamu hadi 'mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu. 
Uzinduzi wa ombi hilo unakuja siku chache kabla ya mkutano wa mawaziri wa kuhusu hali ya kibinadamu ulioandaliwa kufanyika Jumatatu ijayo, Septemba 13 huko Geneva nchini Uswis.  

"Wito huo ni kipaumbele cha mahitaji ambayo hayajatimizwa katika mpango wa hatua za kibinadamu wa mwaka uliozinduliwa mapema mwaka huu, pamoja na mahitaji mapya," amesema Jens Laerke, msemaji shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA katika mkutano wa waandishi wa habari huko Geneva hii leo.  

Ombi hilo linajumuisha dola milioni $ 413 za mahitaji ambayo hayajafadhiliwa ambayo tayari yalikuwa katika ombi la awali, na  dola milioni $ 193 zimetengwa kwa ajili ya mahitaji mapya na mabadiliko ya gharama za uendeshaji, kulingana na OCHA. 

Ukikabiliwa na mahitaji yanayoongezeka nchini humo, Umoja wa Mataifa unatarajia kujitolea zaidi kutoka kwa nchi wahisani.  
Kwa Umoja wa Mataifa , msaada huu wa dola milioni $ 606 unahitajika ili kutoa chakula na kusaidia karibu watu milioni 11 katika miezi minne iliyobaki ya mwaka 2021. 

Martin Griffiths, UN humanitarian chief, discusses humanitarian issues with Taliban leaders in Kabul, Afghanistan. 
Kuporomoka kwa huduma za kimsingi nchini Afghanistan 
"Hii inajumuisha watu milioni mbili ambao hapo awali hawakupata msaada wa  mpango wa hatua za kibinadamu," amesema Laerke.  
Ombi hili jipya litatoa huduma kwa watu milioni 3.4 na kusaidia katika miradi ya mapambano dhidi ya utapiamlo mkali kwa watu milioni moja. 

Pia litaboresha usafi wa mazingira na usafi wa maji kwa watu milioni 2.5.  
Mfumo huo pia unajumuisha sehemu ya ulinzi wa Waafghani milioni 1.5, haswa dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia.  
Mbali ya hayo sehemu ya ombi hilo itafadhili miradi ya elimu ya dharura ya watoto, pamoja na malazi na misaada mingine isiyo ya chakula. 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres atasimamia mkutano wa mawaziri utakaofanyika ana kwa ana na kwa njia ya mtandao kuhusu Afghanistan ambao umepangwa kufanyika Jumatatu ijayo huko Geneva.  
Kulingana na msemaji wa OCHA, nchi hiyo inakabiliwa na kuporomoka kwa huduma za kimsingi.  

Huduma hizi zinaporomoka wakati  huduma zingine kama chakula na misaada mingine muhimu iko karibu kuisha. 
Mkutano huko Geneva kuunga mkono ombi la fedha 
Bwa Laerke amesema "Tunawahimiza wafadhili wa kimataifa kuunga mkono ombi hili haraka na kwa ukarimu. Tukio la Septemba 13 ni fursa ya kujitolea kuunga mkono wito huu." akikumbusha onyo la hivi karibuni kutoka kwa mkuu wa Umoja wa Mataifa juu ya" janga la kibinadamu linalokaribia "nchini Afghanistan. 

Mtoto akiwa katika hospitali ya watoto ya Gandhi mjini Kabul nchini Afghanistan
© UNICEF/Sayed Bidel
Mtoto akiwa katika hospitali ya watoto ya Gandhi mjini Kabul nchini Afghanistan

 

Kulingana na Umoja wa Mataifa, Waafghani milioni 18, au nusu ya wato wote nchini humo, wanahitaji msaada wa kibinadamu.  
Kana kwamba hiyo haitoshi, shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) lina wasiwasi juu ya "kutokuwepo  kwa uhakika wa chakula" na tishio lake kwa maisha ya watu wa vijijini. 
"Hali hii imekuwa wasiwasi mkubwa kwa miezi sasa ," Rein Paulsen, mkurugenzi wa operesheni za dharura za FAO, ameuambia mkutano na waandishi wa habari kutoka Islamabad, Pakistan.  

Uchambuzi wa hivi punde kati ya mwezi (Machi-Mei) kwa Afghanistan uligundua kuwa  mtu mmoja kati ya Waafghan watatu anakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula. 

"Hali ya sasa inasababisha usumbufu mkubwa zaidi  wa upatikanaji wa fedha, masoko, upatikanaji wa pembejeo za kilimo, mikopo na kazi na inatishia msimu muhimu wa ngano wa majira ya baridi nchini Afghanistan, ambao uko njiani. kuanza, ”akaongeza. 

A community in a remote region of Afghanistan depends on mobile clinics run by humanitarian agencies to receive primary health care. Mahitaji ya haraka katika maeneo ya vijijini 
Kulingana na FAO, fursa ya kusaidia wakulima kujiandaa kwa msimu wa ngano na msimu wa baridi inayokaribia ni nyembamba na ina muda mdogo. 

Mamilioni ya watu vijijini Afghanistan wanategemea kilimo kwa maisha yao na uhakika wa chakula nyumbani.  
Asilimia 70% ya Waafghan wanaishi vijijini na kilimo huzalisha asoilimia 25.5% ya Pato la Taifa, moja kwa moja huajiri asilimia 45 ya wafanyakazi na hutoa riziki (moja kwa moja na isiyo ya moja kwa moja) kwa asilimia 80 ya idadi ya watu wa nchi hiyo. 

Kwa FAO, lazima sasa tuongeze misaada ya kimataifa. "Tusipofanya hivi, njaa na watu kutawanywa vitaongezeka kwa muda mfupi na maisha ya familia za vijijini yatapata athari kubwa za muda mrefu," Paulsen ameonya. 

Wakati huo huo, FAO inasalia nchini Afghanistan. Mwezi uliopita wa Agosti ilitoa riziki na msaada wa pesa kwa zaidi ya watu milioni 1.5 katika mikoa 26 kati ya 34 za nchi hiyo.  

Na mwezi Agosti pekee, FAO ilifikia zaidi ya watu 100,000. Licha ya hali tete inayoendelea sasa, FAO iliweza kuendelea na shughuli zake katika majimbo 26 kati ya 34 ya nchi hiyo. 

Msichana waki Afghan alijeruhiwa akiwa shule mjini Kabul wakati wilaya 13 ziliposhambuliwa
© UNICEF Afghanistan
Msichana waki Afghan alijeruhiwa akiwa shule mjini Kabul wakati wilaya 13 ziliposhambuliwa

Zahma ya watoto waliohamishwa kutoka Afghanistan 
Kwa upande mwingine, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF, limeelezea wasiwasi wake juu ya hatima ya watoto wasioandamana na wazazi au walezi na waliotenganishwa na wazazi au walezi ambao wamehamishwa kutoka Afghanistan.  
Hadoi sasa UNICEF na washirika wake wameorodhesha watoto 300 walio peke yao na waliotenganishwa ambao walihamishwa kutoka Afghanistan. 
"Tunatarajia idadi hiyo kuongezeka na juhudi zinazendelea za utambulisho," amesema mkurugenzi mtendaji wa UNICEF Henrietta Fore katikia taarifa yake. 
Tangu Agosti 14, mamia ya watoto wametengwa na familia zao chini ya "hali ya machafuko, pamoja na uhamishaji mkubwa unaoendelea , katika uwanja wa Ndege wa Kabul na maeneo jirani".  
Kulingana na UNICEF, baadhi ya watoto hawa walihamishwa kwa ndege kwenda Ujerumani, Qatar na nchi zingine. 
"Ni muhimu watambuliwe haraka na kuwekwa salama wakati wa mchakato wa kutafuta na kuwaungannisha na familia zao," ameongeza Bi Fore, akisisitiza umuhimu wa "kutanguliza masilahi ya mtoto mbele.”  
Na kulinda watoto dhidi ya dhuluma, kutelekezwa na vurugu "Ninaweza tu kufikiria jinsi watoto hawa walivyokuwa na hofu ya kujikuta bila familia zao ghafla wakati mgogoro ulipojitokeza katika uwanja wa ndege au walipochukuliwa na ndege ya kuwaokoa," Bi Fore. 

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter