Mwanamuziki Lokua Kanza atoa ujumbe kwa wanafunzi nchini DRC
Lokua Kanza, mwanamuziki nguli ndani na nje ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye pia ni balozi wa kitaifa wa elimu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo, ametumia ziara yake katika shule ya msingi aliyosoma utotoni ili kuchagiza wanafunzi wa kike na wa kiume kupatia kipaumbele suala la elimu.