Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wiki ya hali ya hewa Afrika inalenga kuchagiza kasi ya kikanda kuelekea: UNCAC

Wakimbizi huko Minawao, kaskazini mashariki mwa Kamerun, wanapanda miti katika mkoa ambao umekatwa misitu kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa na shughuli za kibinadamu.
© UNHCR/Xavier Bourgois
Wakimbizi huko Minawao, kaskazini mashariki mwa Kamerun, wanapanda miti katika mkoa ambao umekatwa misitu kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa na shughuli za kibinadamu.

Wiki ya hali ya hewa Afrika inalenga kuchagiza kasi ya kikanda kuelekea: UNCAC

Tabianchi na mazingira

Wiki ya vikao vya hali ya hewa barani Afrika 2021 imeanza leo Jumatatu kwa wito wa kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi kutoka kwa sauti muhimu kwenye ukanda huo. 

Katika kikao hicho maalum cha kuanza kwa wiki hiyo katibu mtendaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya hali ya hewa UNCAC Patricia Espinosa ameweka bayana kwamba “Shauku lazima iwe neno linaloongozwa na matendo yetu yote kwani tunakimbizana na wakati”. 

Kwa mujibu wa Bi. Espinosa mkutano huu, ulioandaliwa na serikali ya Uganda kwa msaada wa Umoja wa Mataifa na mashirika kadhaa ya ukanda huo, ni fursa ya kukuza ushirikiano katika changamoto za haraka na kuimarisha mbepo kwa ajili ya wakati wa hatari za mavbadiliko ya tabianchi katika kanda hiyo. 

"Wiki ya hali ya hewa barani Afrika inaongeza kasi ya mafanikio katika mkutano wa COP 26," ameongeza Bi Espinosa, akimaanisha mkutano wa mabadiliko ya tabianchi wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika Glasgow, Scotland, mwezi Novemba mwaka huu. 

Mkutano huo wa wiki ya hali ya hewa unaoendelea hadi Septemba 29, umewaleta pamoja washiriki zaidi ya 4,500, wakijumuisha maafisa wa serikali, viongozi wa biashara na wawakilishi wa asasi za kiraia, kushiriki mazungumzo yenye mwelekeo wa suluhisho na kuonyesha hatua za dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. 

Pia unakusudia kutoa habari juu ya kampeni za UN 'Go Zero' na 'Race to Resilience', zote za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi huku ukihakikisha kuwa sauti za ukanda huo zinasikika katika mchakato wa hali ya hewa unaojumuisha pande nyingi. 

Wiki ya hali ya hewa Afrika inazingatia maeneo matatu muhimu: 

  • Kujumuishwa kwa hatua kabambe katika sekta muhimu za uchumi katika mipango ya kitaifa. 
  • Kukabiliana na hatari za mabadiliko ya tabianchi na kujenga mnepo. 
  • Kutumia fursa za mabadiliko kuuweka ukanda huo kwenye njia ya kupunguza uzalishaji wa gesi chafu ya
Uchafuzi wa hewa kutoka kwenye viwanda vinavyotumia makaa ya mawe unahusika kwenye kuongeza joto la dunia na matatizo mengine ya kimazingira na afya ya umma
Unsplash/Kouji Tsuru
Uchafuzi wa hewa kutoka kwenye viwanda vinavyotumia makaa ya mawe unahusika kwenye kuongeza joto la dunia na matatizo mengine ya kimazingira na afya ya umma

viwandani na maendeleo endelevu. 

Ni swala la suluhu 
Katika miezi ya hivi karibuni, Afrika imeshuhudia mafuriko mabaya, uvamizi wa nzige na sasa inakabiliwa na wimbi la kutisha la ukame kwa sababu ya matukio ya La Niña, amesema naibu msimamizi na mkurugenzi wa Kanda kwa Afrika kutoka shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Ahunna Eziakonwa. 
Amesisitiza kuwa "shughuli za binadamu sasa ndio shughuli kubwa zinazounda dunia yetu".  

Kwake, wiki ya hali ya hewa Afrika ni suala lasuluhu “Najua tunaweza kuckukuna vichwa zaidi na kuibuka upande mwingine na suluhu ambazo zinakwenda sanjari na muktadha wa Afrika," amesema. 

Hatua zilizoimarishwa dhidi ya mabadiliko ya tabianchi 

Wadau wengi wa ukanda huo waliokusanyika wakati wa vikao hivi watawasilisha hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuwasilisha hatua walizopiga kabla ya COP 26 hasa uwasilishaji wa mipango madhubuti ya kitaifa ya mabadiliko ya tabianchi chini ya mkataba wa utabiri wa mabadiliko ya tabianchi na michango iliyoainishwa Kitaifa au (CDNs). 

NDCs ni pamoja na mipango ya kujenga mnepo kwa athari zisizoweza kuepukika za mabadiliko ya tabianchi pamoja na mafuriko ya mara kwa mara, Dhoruba kubwa, moto na ukame. 

Kukamilishwa kwa mipango ya kitaifa ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi imeelezwa kuwa ni muhimu sana kwa Afrika. 

Kulingana na waziri wa maji na mazingira wa Uganda, Sam Cheptoris, bara la Afrika linakabiliwa na mzozo wa vizazi na vizazi, huku kucheleweshwa kwa lengo la kupunguza ongezeko la joto duniani hadi kufikia nyuzi joto 1.5 Celsius, kama unavyosema Mkataba wa Paris, vitakuwa na athari mbaya katika bara hilo. 

"Kukiwa na mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi, Afrika lazima iungane na kuweka mikakati ya ukuaji wa kiwango cha chini ambayo inanufaisha Waafrika wote na ulimwengu wote," amesema Cheptori. 

Mpango mpya wa utekelezaji wa mabadiliko ya tabianchi wa Benki ya Dunia unasaidia hatua za kitaifa na njia za uchumi ili kufanikisha kuwa na mustakbali endelevu, ulio na kiwango kidogo sana cha hewa ukaa na wenye utulivu. 

"Kwa miaka mitano ijayo, asilimia 35% ya ufadhili wa kikanda wa Benki ya Dunia utaenda moja kwa moja kwa hatua za mabadiliko ya tabianchi," amesema Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika Hafez Ghanem. 

Kufanya kazi pamoja ili kujikwamua vyema 

Wiki ya hali ya hewa Afrika ni fursa nzuri ya kubadilishana uzoefu, kujifunza kutoka kwa kila mmoja, na kuhamasishwa kuleta mabadiliko ya kudumu, amesema msimamizi wa programu ya nishati na mabadiliko ya tabianchi katika shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira (UNEP). 

Kwa Mark Radka, "kujikwamua kwa mafanikio ni fursa ya kukua haraka, bora, kulinda mazingira, na kusogea karibu na siku zijazo zilizotawaliwa na mazingira biora na zilizo jumuishi zaidi kwa Afrika yote". 

Ameongeza kuwa "Tunaweza kupata mengi zaidi kwa kufanya kazi pamoja, na wiki ya hali ya hewa Afrika ni fursa nzuri ya kubadilishana uzoefu, kujifunza kutoka kwa kila mmoja na kuhamasishana kufanya kuleta ya kudumu.”