Pamba, kitambaa kinachositiri zaidi ya familia milioni 100 duniani:UN
Leo ni siku ya pamba duniani ikiwa ni maadhimisho ya kwanza kabisa ya siku hiyo kuenzi zao ambalo kitabaa chake kinatengeneza mavazi ya kila siku yaliyosheheni kwenye mkabati mengi ya nguo na ni kitambaa kizuri, rahisi kuvaa, kukitunza na kinadumu kwa muda mrefu. Lakini kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa thamani ya pamba ni zaidi ya kitambaa kama inavyofafanua taarifa ya Flora Nducha