Penye nia pana njia kama nimefika NASA nawe utaweza: Mhandisi Dkt.Alinda Mashiku

Dkt. Alinda Mashiku,mhandisi katika kituo chasafari za anga cha NASA tawi la Goddard Maryland nchini Marekani.
Mwanamke Mtanzania angara kituo cha safari za anga cha Marekani NASA tawi la Goddard mjini Maryland lililojikita na ufuatiliaji wa safari za satellite. Dkt. Alinda Mashiku ambaye amekuwa NASA kwa miaka minane sasa anasema ilimchukua miaka 12 hadi kuajiriwa NASA kama mhandisi na sasa pia ni meneja wa kitengo cha kuhakikisha satellite zonazokwenda angani hazigongani. Je anahisi vipi kuwa miongoni mwa wanawake wachache wahandisi NASA na safari yake ilianza vipi? Kufahamu yote hayo na mengine mengi ungana na Flora Nducha wa UN News Kiswahili aliyeketi na kuzungumza naye katika makala hii