Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa amataifa la wanawake-UN-Women,Phumzile Mlambo-Ngcuka,(kushoto) akiwa na wanawake wmjini Baidoa Somalia.
UN Women/Patterson Siema

Hatuwezi kutothamini mchango wa nusu ya watu duniani :Guterres

Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo kila mwaka huwa Mach inane wito umetolewa kuhakikisha uwezeshaji wanawake na usawa jinsia vitu ambavyo ni muhimu kwa maendeleo ya dunia. Wito huo umetolewa na viongozi mbalimbali wanawake kwenye Umoja wa Mataifa lakini pia Katibu Mkuu Antonio Guterres. Kaulimbiu ya mwaka huu ikiwa ni “fikra sawa, jenga kwa ufanisi na kuwa mbunifu kwa mabadiliko 

Sauti
3'
Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika mgogoro wa jina katika ya Ugiriki na Macedonia iliyokuwa Jamhuri ya Yugoslavia (FYROM), Matthew Nimetz
UN News/Video capture

Kukata tamaa sio hulka yangu: Nimetz

Mwezi Juni mwaka jana mkataba wa kihistoria ulimaliza mgogoro wenye utata wa miaka 27 kati ya nchi mbili, ambazo ni jamhuri ya Yugoslavia ya zamani na Ugiriki. Mwanaume mmoja Matthew Nimetz kwa uvumilivu na hekma aliongoza majadiliano kwa niaba ya Umoja wa Mataifa kwa zaidi ya miongo miwili na akizungumza na UN News amesema Imani yake ya matokeo chanya katika mchakato huo haikuwahi kutoweka.

Sauti
4'16"