Chonde chonde fahamuni nyuki nao wana nafasi yao kwenye uzalishaji wa chakula- Ripoti

22 Februari 2019

Ripoti ya kwanza kabisa kuhusu hali ya baiyonuwai duniani ambayo husaidia kwenye uzalishaji wa chakula imeonyesha kupungua kwa kiasi kikubwa kwa kiwango cha bayonuai.

Ikiwa imeandaliwa na shirika la chakula na kilimo duniani, FAO, ripoti hiyo imechambua hali ya mimea, wanyama na vijidudu ambavyo vinasaidia kwenye uzalishaji wa chakula na mazao ya kilimo.

Ripoti inasema wadudu kama nyuki, udongo, miti na hata vijidudu vidogo zaidi ambavyo haviwezi kuonekana kwa macho ya kawaida vina dhima muhimu katika uzalishaji wa chakula lakini bayonuia ambayo inasaidia uwepo wao iko hatarini na vivyo hivyo uhakika wa chakula kwa binadmau.

Dan Leskien kutoka kamisheni ya rasimali za kijenejitiki za chakula FAO anasema bayonuai ni mchanganyiko wa mimea na wanyama vilivyoko duniani na bila bayonuia tusingalikuwa na chakula chochote na zaidi ya yote,

FAO
Nyuki ni wadudu muhimu sana, bila uwepo wao maua hayatachavuliwa na upatikanaji wa chakula utakuwa hatarini.

"Bayonuai pia ni kiwango kikubwa cha vijidudu vidogo ambavyo havitufikii kwenye sahani ya chakula lakini ni muhimu katika uzalishaji wa chakula. Mfano nyuki tunaohitaji kwa kuchavua maua, vijidudu ambavyo vinatengeneza minyoo au wadudu ambao wanarutubisha udongo na misitu ambayo inahifadhi vyakula vya mwituni na kurekebisha tabianchi na mikoko, majani na matumbawe ambayo ni makazi ya aina mbalimbali za samaki.”

Ametaja vichocheo vya kupungua kwa bayonuai kuwa ni pamoja na mabadiliko ya tabianchi, uchafuzi wa mazingira na shinikizo la kusaka mazao bila kujali athari zake za mazingira akisema  kinachopaswa kufanywa ni..

Tunahitaji kushughulikia hivi visababishi vya kutoweka kwa bayonuai kama vile uchafuzi wa mazingira, matumizi ya rasilimali kupita kiasi, na tabia za walaji. Tunahitaji kuhakikisha tunahifadhi bayonuia popote pale na kwa njia yoyote ile kwa kuitumia kwa uendelevu.”
 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud