Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kukata tamaa sio hulka yangu: Nimetz

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika mgogoro wa jina katika ya Ugiriki na Macedonia iliyokuwa Jamhuri ya Yugoslavia (FYROM), Matthew Nimetz
UN News/Video capture
Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika mgogoro wa jina katika ya Ugiriki na Macedonia iliyokuwa Jamhuri ya Yugoslavia (FYROM), Matthew Nimetz

Kukata tamaa sio hulka yangu: Nimetz

Amani na Usalama

Mwezi Juni mwaka jana mkataba wa kihistoria ulimaliza mgogoro wenye utata wa miaka 27 kati ya nchi mbili, ambazo ni jamhuri ya Yugoslavia ya zamani na Ugiriki. Mwanaume mmoja Matthew Nimetz kwa uvumilivu na hekma aliongoza majadiliano kwa niaba ya Umoja wa Mataifa kwa zaidi ya miongo miwili na akizungumza na UN News amesema Imani yake ya matokeo chanya katika mchakato huo haikuwahi kutoweka.

Kama wasemavyo waswahili kwamba mvumilivu hula mbivu, hatimaye ndoto zake zilitimia pale mkataba wa “Prespa” uliosimamiwa na Umoja wa Mataifa ulipoidhinishwa na Athens na Skopje na mabunge ya nchi hizo mbili na kuanza kutekelezwa rasmi Februari 12 ukitambua rasmi “Jamhuri ya Macedonia Kaskazini.” Kutokana na sababu mbalimbali na pengine majaliwa mkataba huo ulitiwa saini miezi saba kabla na waziri mkuu wa Ugiriki na Macedonia Kaskazini tarehe “17 Juni siku ambayo Nimetz aliadhimisha miaka 79 ya kuzaliwa.”

Nimetz akielezea milima na mabonde ya safari ya mkataba huo na akijiandaa kuachia ngazi kama mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu, jukumu alilolibeba tangu mwaka 1999 kwa kulipwa mshahara wa dola 1 ya Marekani kwa mwaka amesema ni kwa nini imechukua miongo kutimiza lengo

(Sauti ya Nimetz)

“Ni suala ambalo watu wanawaza vipi kutumia muda wa miaka 24 kulenga neno moja tu, au jina moja. Ni vipi watu wasingekubaliana kuhusu jina, jina linapaswa kuchukua muda wa dakika tano, kumi, kumi na tano lakini kuna mambo mengi yanayozingira jina. Sio jina tu, jina lilikuwa kama kilele cha masuala mengi ni dhahiri kwamba lilikuwa ni suala la utambulisho kwa mataifa yote mawili nchi mpya ya Macedonia iliyokuwa Jamhuri ya Yugoslavia na kuibuka na kuchukua nafasi yake katika mataifa ya Balkans. Ni vipi iwe na uhusiano na nchi jirani, katika muktadha huu, Ugiriki,  moja ya nchi jirani na changamoto na nchi zingine majirani.Kwa hiyo suala lenyewe lilikuwa na sehemu ya kihistoria, na hisia.”

Bwana Nimetz amesema suala la historia lilikuwa ni changamoto kwani ilikuwa historia inayozigusa pande zote akisema kuwa historia inakuwa ya kipekee akitolea mfano sanaa ya Mahatma Gandi kuwepo New York ni sawa lakini iwapo Wamarekani watachukulia kwamba Gandhi alikuwaMmarekani basi hiyo itakuwa ni tatizo kwa India, na akatoa mfano wa wakati mmoja ambapo alionekana kama kwamba anapuuza historia ya mataifa hayo.

(Sauti ya Nimetz)

“Kile ambacho kilifanyika ni kwamba nilisema kitu bila kufikiria, kwani wakati mmoja niliwahi kusema jambo lisilo sahihi nikasema kitu cha kumkashifu mvumbuzi Alexander na nikahoji ni kwa nini kila mtu alikuwa anawaza tu kuhusu Alexnder labda ingekuwa bora kuwaza kitu kingine, kila mtu alikasirika nami wale wa uapnde wa Ugiriki na Macedonia iliyokuwa Jamhuri ya Yugoslavia. Nililazimika kuomba radhi na kufuta kauli ya awali na kuutambua mchango wa mvumbuzi Alexander ambaye alifanya mambo makubwa na kueneza utamaduni wa Ugirika kote ulimwenguni kutoka Ugiriki hadi Afghanistan na zaidi”.

Na kuhusu safari ya kufikia jina lililoafikiwa bwana Nimetz amesema,

Patrick Newman
Miaka ishirini na saba kupata jina?

 

(Sauti ya Nimetz)

Kwa hiyo nilitoa mapendekezo matano, ikiwemo Jamhuri ya Marcedonia Kaskazini, ambalo hatimaye lilikubalika, jamhuri ya Macedonia ya juu, jamhuri ya Macedonia mpya na nikasema hapa kuna majina matano ni mazuri na ni ya heshima kwa sababu suala lilikuwa kwamba Macedonia ni eneo kubwa na nchi ni sehemu ya eneo sio eneo lote. Kwa hiyo, kutokana na mtazamo wa Kigiriki, ikiwa unajiita Jamhuri ya Macedonia unamaanisha eneo hilo lote ni lako.”

Bwana Nimetz akihitimisha mazungumzo yake na UN News amesema amefanya kazi hiyo kwa muda mrefu na kwamba mbali ya  kwamba yamefikiwa makubaliano ya Prespa sasa utekelezaji wake ni muhimu.