Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viumbe vya majini vina mchango mkubwa katika mustakabali wa dunia :UN

Nyangumi  huko kaskazini mwa Thailand. Kaulimbiu ya mwaka huu ni: 'Maisha chini ya maji: kwa ajili ya watu na sayari'
UNDP Thailand
Nyangumi huko kaskazini mwa Thailand. Kaulimbiu ya mwaka huu ni: 'Maisha chini ya maji: kwa ajili ya watu na sayari'

Viumbe vya majini vina mchango mkubwa katika mustakabali wa dunia :UN

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Viumbe vya majini vina mchango mkubwa katika mustakabali wa malengo ya maendeleo endelevu na sayari dunia, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP, na ndio maana kauli mbiu ya siku ya wanyama pori duniani Machi 3 mwaka huu ikamulika maisha hayo ikisema "Maisha chini ya maji:kwa ajili ya watu na sayari. ’’

Kwa mujibu wa UNEP kauli mbiu hiyo inamaanisha  jukumu kubwa la viumbe hivyo kimataifa katika masuala ya uhakika wa chakula, kutokomeza umasikini na ustawi wa maisha ya binadamu katika nchi kavu. Katika kupitisha lengo namba 14 la maendeleo endelevu yaani SDGs, dunia iliahidi “kulinda na matumizi endelevu ya bahari na rasilimali zake. ‘’

Lengo kuu la kaulimbiu ya siku hii

UNEP inasema lengo kuu la kaulimbiu ya mwaka huu ni kuelimisha kuhusu bayoanuai ya maisha ya majini na umuhimu wa viumbe vya majini kwa maendeleo ya binadamu na pia kutafiti ni jinsi gani tutahakikisha kwamba baharí zetu zitaendelea kutoa huduma hizo muhimu kwa vizazi vijavyo.

Zimeongeza kuwa maji yakiwa yamefunika theluthi mbili ya dunia baharí zinatoa asilimia 50 ya hewa ya oxygen duniani, yanadhibiti hali ya hewa , kutoa chakula kwa zaidi ya watu bilioni 3 na kuchukua zaidi ya asilimia 30 ya hewa ukaa inayozalishwa hewani na asilimia 90 ya joto litokanalo na mabadiliko ya tabia nchi. Licha ya faida zote hizo bado shughUli za binadamu zinatishia mazingira haya muhimu.

Hatua za kulinda mazingira ya bahari

Kama sehemu ya hatua mbalimbali zinazochukuliwa kwa ajili ya siku hii ya wanyama pori duniani UNEP inasema kampeni kwa ajili ya maisha ya wanyama pori inawatambulisha watu wapya mashuhuri 16 na aina mpya ya viumbe vya baharini vikiwemo papa wa mbegu, papa aina ya mako, nyangumi, taa, kiwi au penguini, dubu wanchi ya Kaskazini na matumbawe. Mabalozi hawa wapya wanajumuisha wapiga picha wa wanyana pori na watu wengine maarufu wenye jumla ya wafuasi milioni 320 kwenye mitandao ya kijamii na kuungana na timu ya mabalozi wema wa mazingira wa akiwemo Umoja wa Mataifa Adrian Grenier na Aidan Gallagher ambao ni vinara wa samaki na Gisele Bundchen aliyeasili kasa kama myama wake.

Samaki aina ya Taa akihangaika katika eneo la Bali lililochafuliwa na plastiki, Indonesia.
UN World Oceans Day/Joerg Blessing
Samaki aina ya Taa akihangaika katika eneo la Bali lililochafuliwa na plastiki, Indonesia.

 

Uhifadhi wa viumbe vya baharini ni wajibu wa kila mtu

Kwa mujibu wa UNEP kila mmoja na wajibu wa katika kulinda viumbe vya baharini na kama unataka kuhakikisha vinaisho basi ni lazima uepuke kununua vyakula, vifaa vya urembo , sanaa na dawa za asili za Asia ambazo zinatumia viungo vya mwili vya viumbe hivyo, badala yake chagua kutumia vyakula endelevu vitokanavyo na viumbe vya baharini na bila shaka achana m na matumizi ya mara moja ya bidhaa za plastiki kwani sasa ni wajibu wetu kuhakikisha viumbe hivyo vinasalimika.

Akiunga mkono hoja hiyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Martaifa Antonio Guterres katika ujumbe wake wa siku hii anasema watu bilioni 3 wanategemea baharí na bayoanuai ya majini kwa ajili kujikimu kimaisha na kwamba sekta ya baharí na rasilimali za pwani zinaingiza dola trilioni 3 za Marekani kila mwaka ikiwa ni sawa na asilimia 5 ya pato la dunia.

Taka za plastiki katika bahari za ni tisho kwa viumbe wa majini
Saeed Rashid
Taka za plastiki katika bahari za ni tisho kwa viumbe wa majini

 

Matumaini ya kuokoa viumbe vya majini

Guterres anasema hivi sasa maisha ya viumbe  baharini yako katika shinikizo kubwa kuanzia mabadiliko ya tabianchi hadi uchaguzi wa mazingira , kutoweka kwa makazi ya mwambao na uvuvi wa kupindukia ambapo theluthi moja ya akiba ya samaki wa biashara wametokana na uvuvi wa kupindukia na viumbe wengine kama kasa wanaanza kutoweka kutokana na matumizi ya kupindukia ya rasirimali za baharini.

Hata hivyo habari Njema ni kwamba suluhu ipo amesema Katibu mkuu kwa mfano mahali ambapo uvuvi unadhibitiwa kisayansi kuna fursa kubwa ya kurejea kwa akiba ya samaki. Na sasa mkataba kuhusu biashara ya kimataifa ya viumbe vilivyo hatarini na mimea (CITES) unaongeza sheria kuhusu viumbe vya baharini na mkataba kuhusu bayoanuai (CBD) unashirikishwa katika kuandaa mkakati wa wa kimataifa wa bayoanuai baada ya 2020.

Wazamiaji nchini Madagascar
UNDP/Garth Cripps
Wazamiaji nchini Madagascar

Changamoto za sekta ya bahari

Naye mkutugenzi mtendaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu UNODC, Yury Fedotov amesema sekta ya uvuvi inakabiliwa na changamoto nyingi haramu , baharini n anchi kavu kuanzia rushwa, ubadhilifu, usambazaji wa fecha haramu hadi usafirishaji haramu wa binadamu na uny’ang’anyi wa maisha ya viumbe wa majini.

Ameongeza kuwa uhalifu katika sekta ya uvuvi umekuwa ni mfumo wenye faida kubwa kwa uhalifu wa kupangwa ambao hivi sasa unatishia matumizi endelevu ya rasilimali za majini na kuleta athari kubwa katika maendeleo na uchumi wa kimataifa. Amesema UNODC inashikiriki kiamilifu katika kuzisaidia nchi wanachama kuapambana na uhalifu mwingi unaofanyika katika sekata ya uvuvi hasa kwa kupanya kazi kwa karibu na mifumo na taasisi za sheria , malaka za uvuvi na wadau wengine kuboresha mifumo ya sheria iweze kupambana na uhalifu uhusianao na masuala ya uvuvi, lakini pia kuchagiza uwajibikaji kwa ajili na matumizi endelevu ya rasilimali na kulinda maisha ya mamilioni ya watu ulimwenguni.