Hatuwezi kutothamini mchango wa nusu ya watu duniani :Guterres

8 Machi 2019

Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo kila mwaka huwa Mach inane wito umetolewa kuhakikisha uwezeshaji wanawake na usawa jinsia vitu ambavyo ni muhimu kwa maendeleo ya dunia. Wito huo umetolewa na viongozi mbalimbali wanawake kwenye Umoja wa Mataifa lakini pia Katibu Mkuu Antonio Guterres. Kaulimbiu ya mwaka huu ikiwa ni “fikra sawa, jenga kwa ufanisi na kuwa mbunifu kwa mabadiliko 

Katika ujumbe wa pamoja kwa ajili ya siku hii , na kwa kutambua umuhimu na mchango wa wanawake Guterres amesema

 

(SAUTI YA ANTONIO GUTERRES)

kwa mara ya kwanza Umoja wa Mataifa umefikia uwiano wa kijinsia kwenye uongozi wa juu wa Umoja huo na miongoni mwa nafasi za uongozi za Umoja wa Mataifa kwingineko duniani na lengo ni kutimiza uwiano huo ndani ya muongo mmoja

Akiunga mkono hilo naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed amesema wanawake ni kundi kubwa lisiloweza kupuuzwa

(SAUTI YA AMINA MOHAMMED)

"Usawa wa kijinsia ni muhimu ili kuleta ufanisi kwenye kazi zetu, na hatuwezi kupoteza mchango wa nusu ya idadi ya watu duniani. Na ushiriki sawa wa wanawake kwenye nguvu kazi kutafanikisha dola trilioni kwenye maendeleo ya duniani. Hebu tueleweke hatuewzi kujenga mustakabali tunaotaka wa kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu bila ushiriki kamilifu wa wanawake.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed akiwa ofisini kwake kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York
Picha UN News /Matt Wells
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed akiwa ofisini kwake kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji UN Women Phumzile Mlambo Ngucka amesema pamoja juhudi hizo

(SAUTI YA PHUMZILE MLAMBO NGUCKA)

"Lakini bado wanawake na wasichana duniani kote wanakumbwa na changamoto. Katika siku ya wanawake duniani, tunawasihi nyote muungane nasi fikra sawa, jenga kwa ufanisi na kuwa mbunifu kwa mabadiliko”.

Akisisiza lengo la kuongeza idadi ya wanawake kwenye madaraka Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Maria Fernanda Espinosa anafunguka

(SAUTI YA MARIA FERNANDA ESPINOSA)

Na tunahitaji wanawake wengi zaidi viongozi washiriki kwenye masuala ya umma na kupitisha maamuzi.  Heb una tuongeze juhudi zetu maradufu dhidi ya ubaguzi na ukatili ambao wanawake na wasichana wanakabiliwa nao kila siku.  Hebu tuongeze juhudi kwa usawa wa jinsia na kuhakikisha kuwa hakuna mwanamke au msichana anaachwa nyuma"

Na akigusia changamoto zinazowaghubika vijana duniani mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu kuhusu vijana Jayathma Wiramanayake amesema

(JAYATHIMA WICRAMANAYAKE)

Vijana wa Afrika wako mstari wa mbele katika ujasiriamali kama inavyoonekana pichanihuko Gambia walipotembelewa na mjumbe maalum wa UN kuhusu vijana, Jayathma Wickramanayake (kulia)
Alhagie Manka/ UNFPA Gambia
Vijana wa Afrika wako mstari wa mbele katika ujasiriamali kama inavyoonekana pichanihuko Gambia walipotembelewa na mjumbe maalum wa UN kuhusu vijana, Jayathma Wickramanayake (kulia)

“Mamilioni ya wasichana vijana wanajiandaa kuanza maisha ya kufanya kazi. Lakini mara nyingi wengi wao hawapati fursa ya kuchanua na kufikia ndoto zao na kuwa na uthabiti. Tunapaswa kubadili hili.! Hebu na tuwekeze kwenye elimu ya wasichana na stadi ili waweze kuwa viongozi na wabunifu ambao wamezaliwa wawe.”

Akihitimisha ujumbe wake Katibu Mkuu amesema wanawake viongozi ni mfano muhimu na anajivunia kufanya kazi na wanawake wabunifu na wenye ari kila siku wakipeleka Umoja wa  Mataifa katika zama mpya.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter